Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Bernard Kibesse (wapili kulia) akiwa ameshika nembo ya Benki mpya ya NBCA Bank Tanzania Limited pamoja na Mkurugenzi Mkuu mteule wa NCBA Bank Limited, Margaret Karume (kulia), Mkurugenzi mteule wa Wateja Wakubwa, Binafsi na Wafanyabiashara wadogo na wa kati wa NCBA Bank Limited, Gift Shoko (kushoto) na Mwenyekiti mteule wa Bodi ya NCBA Bank Limited, Sharmapal Aggarwal kwenye hafla ya uzinduzi wa Benki hiyo uliofanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Mkurugenzi mteule wa Wateja Wakubwa, Binafsi na Wafanyabiashara wadogo na wa kati wa NCBA Bank Tanzania Limited, Gift Shoko akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa logo mpya kuashiria kuanzishwa kwa Benki mpya ya NCBA itakayoanza kutoa huduma rasmi kuanzia tarehe 8 ya mwezi huu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Bernard Kibesse (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu mteule wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume (wapili kulia), Mkurugenzi mteule wa Wateja Wakubwa, Binafsi na Wafanyabiashara wadogo na wa kati wa NCBA Bank Limited, Gift Shoko na Mwenyekiti mteule wa Bodi wa Benki hiyo, Sharmapal Aggarwal mara baada ya uzinduzi wa Benki mpya ya NCBA uliofanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu mteule wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa logo mpya kuashiria kuanzishwa kwa Benki mpya ya NCBA itakayoanza kutoa huduma rasmi kuanzia tarehe 8 ya mwezi huu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar Es Salaam leo
NCBA Bank Tanzania Limited (NCBA) imeonyesha nembo yao mpya na kauli mbiu wakati ilipozindua huduma zao rasmi baada ya kuungana kwa NIC Bank Tanzania Limited (NIC Bank) na Commercial Bank of Africa Tanzania Limited (CBA).
Hii ni kufuatia idhini iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kuunganisha benki hizi mbili na kuzipatia kibali cha biashara kuanzisha huduma zao rasmi tarehe 8 Julai 2020 kama NCBA Bank Tanzania Limited.
Idhini ya mdhibiti na utolewaji wa leseni na Benki Kuu ya Tanzania imetoa njia kwa NCBA Bank Tanzania Limited kuanzisha huduma zake rasmi.
Mwenyekiti mteule wa Benki ya NCBA Tanzania Bw Sharmapal Aggarwal alisema, ‘Benki ya NCBA ni benki imara na kubwa yenye nguvu ya kifedha, utaalamu na muunganiko wa kikanda inayowapatia wateja wake bidhaa na huduma mbalimbali’’.
Alielezea kuwa Benki ya NCBA inahamasisha ukuaji kupitia uvumbuzi wa kidijitali ili kuwapa watu msukumo wa kufanya mambo pasipo kurudi nyuma. Benki inathamini mahusiano binafsi na wateja ili kuleta mafanikio, inatoa huduma na bidhaa kwa upana zenye daraja la kwanza kwa wateja wa aina tofauti; binafsi, biashara na mashirika.
‘Malengo ya Benki ya NCBA ni kuendesha ufanisi na kuendeleza mabadiliko. Ni benki ya kila mtu mwenye ujasiri wa kufika mbali, wenye msukumo binafsi, na wale wenye hamasa wa kufanya mambo yatokee’ aliongezea.
Mkurugenzi Mkuu mteule Bi Margaret Karume alisema kuwa utambulisho wa benki yao mpya utaruhusu ujumuishwaji wa nguvu, maadili na historia za benki za zamani.
‘Tunayofuraha kuwaonyesha nembo yetu mpya ya ujasiri, na ya kuhamasisha kama sehemu ya safari yetu ya uunganaji chini ya bendera moja ya umoja wetu. Nembo yetu inaashiria mizizi na uzoefu wetu wa kikanda. Kuanzia leo, nembo mpya ya Benki ya NCBA na muonekano wake zitatolewa hatua kwa hatua kwenye kila nyanja zinazotumiwa na wateja wetu. Kwenye mwezi mmoja ujao tutakuwa tunabadilisha alama kwenye matawi yetu na taarifa zetu kuakisi utambulisho wetu wa benki’. Alizungumza
Alieleza kuwa jina na nembo ya Benki ya NCBA inaakisi mizizi mirefu na uzoefu nchini Tanzania na kanda kwa ujumla. Inaashiria pia malengo ya benki na NCBA Group kuwa benki inayoongoza Tanzania na bara zima la Afrika.
Kufuatia uunganaji huu, Benki sasa ipo kwenye daraja la pili kwenye taasisi za kibenki inayotoa huduma na bidhaa pana huku ikijipatia nguvu kutoka benki zilizopita.
Benki ipo kwenye hatua za mwisho za uunganaji wa mifumo yake ili wateja waendelee kufurahia huduma kirahisi kwenye nyanja zote hapa Tanzania.
‘Lengo letu hadi kufikia robo tatu yam waka wa 2020, wateja wote wa benki ya NCBA wapate huduma sawa kwenye za viwango vyote bila kujali mahusiano yao ya zamani na benki ya NIC au CBA,’ Bi Karume alisema.
Uunganaji wa biashara za NCBA Group nchini Uganda, Kenya na Rwanda umekamilika.
NCBA Bank Group PLC ina mtandao wa huduma zake katika matawi Zaidi ya 100 kwenye nchi tano ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Ivory Coast. Inahudumia wateja zaidi ya milioni 40 million, Benki ya NCBA ndio kubwa zaidi barani Africa kwa idadi ya wateja.
Mwezi unaofuatia benki itamalizia kujenga upya alama zake kwenye matawi yake ya mikoani kama vile ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments