TBA yajivunia kuingia katika uchumi wa Kati kwa kuwa na mchango. | ZamotoHabari.


*Wampongeza Rais Magufuli kwa kuifikisha nchi katika uchumi wa Kati

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Wakala wa  Majengo  nchini (TBA)umesema kuwa katika hatua ya Tanzania kufika katika uchumi wa Kati unatokana na wakala huo kushiriki ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Akizungumza katika maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Afisa Uhusiano wa TBA Renatus Sona amesema wakala wamekuwa na miradi mingi ambayo inajengwa kwa ubora kutokana na weledi uliojengeka katika kuhakikisha nchi inakwenda katika miundombinu bora.

Amesema kuwa licha ya kuwa na mafanikio hayo  Rais Dkt.John Pombe Magufuli ndio amefanya kuweza kuweza kupata mafanikio hayo ya kuhakikisha miundombinu yote inajengwa kwa ubora.
Sona amesema kuwa watanzania waendelee kuwa bega kwa bega na TBA katika kuwaletea maendeleo katika ujenzi .

Nae Mhandisi wa TBA Pelagia Richard amesema kuwa TBA ina mitambo ya kisasa katika suala la ujenzi kwa kuzingatia viwango vilivyoanishwa.

Amesema kuwa katika miradi ya ujenzi wanachukua tahadhari zote ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa vya usalama katika ujenzi.

Kwa upande wa Afisa Miliki Sara Mbepo amesema kuwa Wana miradi nyumba maeneo mbalimbali ambazo zingine zimeisha na zingine zikiendelea kujengwa.

Amesema nyumba katika eneo la bunju jijini Dar es  Salaam zilishakamilika na bei za nyumba zinauzwa kwa viwango tofauti kutokana na kila mtu anavvyohitaji.

 Afisa Uhusiano wa Wakala Majengo Nchini (TBA) Renatus Sona akizungumza na michuzi media kuhusiana miradi mbalimbali ya ujenzi ya wakala huo katika maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mhandisi Ujenzi wa TBA Pelagia Richard akizungumza kuhusiana na ubora wa ujenzi katika miradi ya TBA kwa kuzingatia viwango kwenye maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Afisa Miliki wa TBA  Sara Mbepo akitoa maelezo kuhusiana na miradi ya nyumba zinazojengwa na zilizokamilika na kuwa sokoni katika maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Wanachi wakipata maelezo ya katika Banda la TBA Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini