NAACOPHA YATOA ELIMU YA VVU KWA VIONGOZI WA DINI. | ZamotoHabari.


NA FARIDA SAIDY-MOROGORO

KATIKA kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi na unyanyapaa katika familia za watu wenye maambukizi ya virusi hivyo, Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA) limetoa Elimu kwa viongozi wa Dini namna watakavyoweza kuisaidia serikali na jamii kwa ujumla katika kupunguza na kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi Nchini.

Akizungumza kwenye semina iliyowakutanisha Viongozi wa Dini kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mratibu wa mwitikio wa viongozi wa Dini kutoka NACOPHA Jovini Riziki amewakata viongozi hao wa Dini kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapiga vita swala zima la unyanyapaa kwa watu wenywe Virusi vya Ukimwi (VVU) wanakuwa katika Nyumba za ibada swala ambalo litasaidia kupunguza kuongezeka kwa maambukizi mapya ya virusi hivyo.

Hata hivyo ameongeza kuwa unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU umekuwa kikwazo kikubwa kinachosababisha hofu kwa watu kwenda kupima  na waliopima kuhofia kwenda kwenye vituo vya kuchukulia dawa na  kuathiri juhudi za kutokomeza maambukizi mapya ya  VVU hapa nchini, hivyo viongozi wa dini wananafasikubwa ya kuwatoa hofu watanzania juu ya swala zima la upima na utumiaji wa dawa VVU.

Aidha ameitaka Jamii hususani wanaume kujitokeza kupima virusi vya Ukimwi kwani tafiti zinaonyesha kuwa ni wanaume wachache wanaojitokeza kupima na kuanza kutumia dawa ikilinganishwa na makundi mengine,jambo linalosababisha kuwa na idadi kubwa ya watu wasiojua Afya zao na kupelekea kuongezeka kwa Maambukizi ya VVU.

Wakizunguza kwa nyakati tofauti viongozi hao wa dini akiwemo Father EMIL DEOGRATIAS KOBERO mlezi wa vijana Jimbo katoliki Morogoro wamesema wao kama viongozi wa Dini wamejipanga na wapo tayali kusimamia mapambano dhidi ya  unyanyapaa unaodumaza juhudi za kutokomeza maambukizi ya VVU na ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto.

Aidha  Kupitia mradi wa HEBU TUYAJENGE unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani (USAID)wenye lengo la kuhimiza jamii kuongeza utumiaji sahihi wa huduma za Ukimwi katika maeneo yao,matunzo na tiba kwa makundi yalio katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa VVU hasa wasichana na wanawake wa kati, viongozi wa Dini nchini kwa pamoja wametia sahihi azimio la mwitikio wa Taifa wa kutokomeza Unyanyapaa dhidi ya Virusi vya Ukimwi na ukatili wa kijinsia kwa watoto, jambo ambalo limeleta mwanga katika kufikia malengo ya Tanzania bila ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi ifikapo 2030.

Hata hivyo Tanzania inakadiriwa kuwa na wastani wa watu million 1.6 wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, kati yao theluti mbili pekee ndio wanaotambua wana maambukizi, huku wengine wakiishi bila kujua hali zao, hivyo kuendelea kuwaambukiza wengine, huku viongozi wa Dini wakitazamwa kuwa dira, kuifikia Tanzania bila maambukizi mapya ifikapo 2030.
 
 .Father  EMIL DEOGRATIAS KOBERO mlezi wa vijana Jimbo Katoliki Morogoro akimuelekeza jambo Mratibu wa mwitikio wa viongozi wa Dini kutoka NACOPHA Jovini Riziki baada ya kumaliza semina iliyowakutanisha  viongozi wa dini kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la MOROGORO.
 Viongozi wa Dini wakiwa katika picha ya pamoja mala baada ya kupata semina ya namna watakavyo kabiliana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi hapa nchini.




APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini