Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, amempongeza Rais Magufuli pamoja na Watanzania kiujumla, kufuatia ripoti ya Benki ya Dunia iliyoitaja Tanzania kama imefikia kuwa nchi yenye uchumi wa kati na kuwashangaa wale wote wanaobeza hatua hiyo na kudai kuwa ni wagonjwa wa akili.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 12, 2020, wakati akizungumza kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Rais Magufuli Ikulu ya Chamwino Dodoma, ambayo aliwaalika Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.
"Mh Rais naomba niseme kwa dhati nikupongeze wewe pamoja na Watanzania kiujumla, kutokana na ile taarifa ya Benki ya Dunia ya kwamba Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati, si jambo dogo naona kwenye mitandao wanabeza na mimi nikasema nadhani ni wagonjwa wa akili, tumetoka katika ile hatua ambayo tulikuwa tunatazamwa kama nchi maskini" amesema Waziri Mstaafu.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments