Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglicana Tanzania, Maimbo Mndolwa, amewataka wanasiasa kuacha tabia ya kuingiza siasa kwenye nyumba za ibada, badala yake wayavue makoti yao ya siasa pindi wanapoingia kwenye nyumba hizo ili kuendelea kuidumisha amani iliyoachwa na waasisi wa nchi.
Kauli hiyo ameitoa akiwa Jijini Mwanza wakati wa ibada maalumu ya kuliombea Taifa, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicholas, na kusema kuwa kwenye viwanja vya siasa kukichafuka, machafuko hayo huhamia kanisani.
"Enyi waumini mlio wanasiasa tuwaombe mnapooingia kanisani makoti yenu ya siasa yaacheni mlangoni, ingieni kama waumini kwa unyenyekevu mkijua kanisani ndipo mamlaka yake, mamlaka za nje zitumike huko, tusidhalilishane, kuoneana na tusilete kejeli za viwanjani na vijiweni kanisani kwa sababu ya siasa, kanisani ni mahali pa kumuabudu Mungu" amesema Askofu Mndolwa.
Katika hatua nyingine Askofu Mndolwa akawataka wagombea wanawake kuacha kutumia miili yao kwa ajili ya kupata uongozi, na badala yake wafate taratibu na kanuni zilizowekwa ili waweze kuwa viongozi wenye kutambua majukumu yao na kuwa na hofu ya Mungu.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments