Kitabu cha Mary Trump, ‘Too Much and Never Enough’: How My Family Created the World’s Most Dangerous Man, kinamuelezea mjomba yake kama mlaghai na mnyanyasaji.
Hatahivyo Ikulu ya Marekani imekanusha madai yaliyomo ndani ya kitabu hicho, dondoo ambazo zimevujishwa na vyombo vya habari vya Marekani.
Familia ya Trump imewasilisha kesi mahakamani ikitafuta kuzuia kuchapishwa kwa kitabu hicho Julai 14.
‘Zaidi ya mbinafsi’
Mpwa wake Trump, 55 anamueleza mjombake kama, ‘hakuna kitakachomtosha’, na kwamba Rais wa Marekani anaonesha sifa zote za mtu mbinafsi.
“Hii ni zaidi ya ubinafsi wa kawaida,” mpwa wake mwenye shahada ya daktari katika Saikolojia ya Kimatibabu, anaeleza kuhusu Trump.
“Donald sio tu kwamba ni mdhaifu, kiburi chake ni kitu asichoweza kukimudu binafsi na kinachohitajika kuimarishwa kila wakati kwasababu ndani ya moyo wake anafahamu fika kwamba yeye sio yule anayedai kuwa.”
Anasema kwamba rais alishawishika kwa kumtazama baba yake, Fred Trump Sr, akimnyanyasa baba yake Fred Trump Jr – aliyekufa kwa maradhi yenye kuhusishwa na pombe.
The Trump family siblings
Picha ya kitambo ya ndugu za Trump, kutoka kushoto kuelekea kulia: Robert, Elizabeth, Fred, Donald na Maryanne
Mary anaandika kwamba Trump Sr alikuwa mkali sana kwa mtoto wake wa kiume mkubwa (yaani baba yake), ambaye alitaka achukue majukumu ya kusimamia biashara ya familia ya uuzaji wa nyumba. Lakini kadiri baba yake Mary alivyokuwa anaendelea kujitenga na maswala ya biashara ya familia, Trump Sr, hakuwa na la kufanya zaidi ya kukimbilia kwa kijana wake mdogo, Donald.
Halikuwa chaguo la kufurahisha, Bi. Trump anasema.
“Mambo yalipoanza kwenda mrama mwishoni mwa miaka 1980, Fred alishindwa kujitenganisha na ukatili na udhaifu wa kijana wake na akalazimika kuendelea kushikilia biashara,” ameandika kuhusu tabia ya Trump Sr, kwa rais wa 45 wa Marekani.
“Jinamizi wake alikuwa huru.”
Ikulu ya Marekani ilikanusha madai kwamba baba yake Trump alikuwa mkali, akisema kuwa rais anaelezea uhusiano aliokuwa nao na baba yake kama wa amani na kwamba baba yake alikuwa mzuri sana kwake”.
‘Ni lazima nimfichue Trump’
Katika kitabu hicho, Bi. Mary anaelezea vile alivyowasilisha nyaraka za kodi kwa gazeti la New York Times, iliyozitumia kuchapisha makala ya uchunguzi ya maneno 14,000 kwa mifumo ya kodi ya miaka ya 1990 ya Trump ikiwemo ulaghai, ambao uliongeza utajiri aliopata kutoka kwa wazazi wake.
Bi. Mary alisema wanahabari walimtafuta nyumbani kwake wakitaka kusema nae 2017 lakini awali, hakuwa tayari kutoa ushirikiano.
Alichukua kipindi cha mwezi mzima, kufuatilia jinsi hali ilivyo wakati ambapo Donald Trump anafanya mambo tofauti na utamaduni uliozoeleka, akihatarisha miungano mbalimbali na kukandamiza walio katika hatari,” kabla ya kuamua kuwasiliana na mwanahabari wa gazeti la New York Times.
Donald and Fred Trump in 1988 at The Plaza Hotel in New York City
Donald na baba yake, Fred, 1988 katika hoteli ya ‘The Plaza Hotel’ mjini New York
Baada ya kupata kimagendo makasha 19 ya nyaraka za sheria kutoka kwa kampuni moja ya sheria zilipokuwa zimewekwa, akazikabidhi kwa wanahabari.
Anaelezea kipindi hicho kama kilichompa faraja ambayo hajawahi kuipata maishani kwa miezi kadhaa.
“Haikutosha kujitolea kusaidia shirika la wakambizi la Syria,” ameandika. “Ilikuwa ni lazima nimfichue na kumdhalilisha Donald.”
‘Alidanganya kuingia chuo kikuu’
Bi. Mary anadai kwamba mjomba wake alimlipa rafiki yake ili amfanyie mtihani kwa niaba yake – mtihani wa kitaifa ambao unaamua chuo kikuu mtu atakachokwenda kwasababu alikuwa na wasiwasi kwamba alama zake za wastani ambazo zingekatiza juhudi zake za kukubaliwa.
“Alitafuta mtu ambaye ni mwerevu na mwenye sifa ya kupita mtihani kumfanyia mtihani kwa niaba yake,” ameandika: “Donald, ambaye hakuna siku alikosa pesa, alimlipa mtu huyo vizuri.”
Bwana Trump alisajiliwa Chuo Kikuu cha Fordham mji wa New York lakini baadae akahamishwa shule ya biashara ya Wharton chuo kikuu cha Pennsylvania.
Ikulu ya Marekani imekanusha kwamba rais alitumia njia za udanganyifu katika mtihani wa kujiunga na chuo kikuu.
Donald aliharibiwa na baba yake
Ms Bi. Mary analaumu familia ya Trump, Fred Trump Sr kwa matatizo mengi katika familia hiyo. Anasema kwamba Trump Sr, tajiri wa biasha ya kuuza nyumba “alimharibia” Donald Trump kwa kuingilia uwezo wake kukua kwa kupata hisia zote za mwanaamu.
“Kwa kumuwekea kipimo Donald kufikia hisia zake mwenyewe na kuzichukulia hisia zake nyingi kama zisizokubalika, Fred aliharibu mtazamo wa kijana wake kuhusu dunia na pamoja na uwezo wake wa kuishi maisha yake,” ameandika.
“Kuwa mkarimu ni jambo ambalo halingewezekana,” kwa Trump Sr, mary ameandika, na kuongeza kwamba angekuwa na hasira kila baba yake – aliyejulikana kama Freddy – angeomba msamaha kwa kosa lolote.
Fred Sr, anasema “angemkejeli. Fred alitaka kijana wake mkubwa kuwa muaji.”
Donald Trump, ambaye ni mdogo kwa miaka saba kwa kaka yake aliyeaga dunia, “alikuwa na wakati mwingi kujifunza kupitia Fred aliyemfedhehesha kijana wake mkubwa, Bi Mary ameandika.
Tatizo la wanawake
Bi. Mary amesema kwamba Donald Trump ambaye ni mjomba wake aliwahi kumuomba aandike kitabu kumhusu kisicho na ukweli wowote, na kumuelezea mkusanyiko wa mambo ya kuhuzunisha kuhusu wanawake aliotarajia kuwachumbia lakini baada ya kumkataa wanawake hao waligeuka na kuwa wabaya zaidi duniani, wenye sura mbaya, walionenepa, na wasiokuwa na maana yoyote kuwahi kukutana nao maishani mwake”.
Na baadae kuna mwanamke mmoja aliyemfuta kazi na hakuwahi kumlipa kwa kazi aliyokuwa ameshafanya, Mary anadai hivyo.
Anasema, Bwana Trump aliusema vibaya mwili wa mwanamke huyo alipokuwa na umri wa mika 29 hata ingawa yeye ni mpwa wake na wakati huo Bwana Trump alikuwa ameoa mke wake wa pili, Marla Maples.
Ameongeza kwamba Bwana Trump alimuarifu mke wake wa sasa Melania kwamba mpwa wake yaani Mary, hakumaliza masomo ya chuo kikuu na pia alitumia madawa ya kulevya wakati alipokuwa amemchukua kwa ajili ya mradi wa kuandika kitabu.
Ni kweli kwamba Bi. Mary alicha chuo lakini anasema hajawahi kutumia madawa ya kulevya na kwamba anaamini kuwa mjomba wake alitunga maneno hayo ili yeye aonekane kama mwokozi wake.
“Simulizi hiyo ilikuwa ni kwa manufaa yake mwenyewe,” ameandika.
Mary Trump ni nani?
Mary Trump, 55, ni binti ya Fred Trump Jr, raia wa kaka mkubwa aliyekufa 1981 akiwa na umri wa miaka 42.
Kaka yake mkubwa Donald, alikuwa na wakati mgumu kukabiliana na unywaji wa pombe kupindukia katika kipidi kirefu cha maisha yake na kifo chake cha mapema kilichosababishwa na mshtuko wa moyo kunahusishwa na unywaji wa pombe.
Rais Trump amezungumzia matatizo binafsi ya kaka yake kama kichocheo cha utawala wake kutafuta suluhu ya kukabiliana na janga la utumiaji wa dawa za kulevya.
Katika mahojiano mwaka jana na gazeti la Washinton Post, Bwana Trump alisema anajutia kumshinikiza kaka yake kujiunga na biashara ya familia ya uuzaji wa majengo.
Mary Trump amekuwa akiepuka vyombo vya habari tangu mjomba wake alipokuwa rais, ingawa siku za nyuma alikuwa mkosoaji wake mkubwa.
Baada ya Bwana Trump kushinda uchaguzi wa urais 2016, anaelezea tajriba yake kama usiku mbaya zaidi katika maisha yake,” kulingana na gazeti la Washington Post.
“Tunastahili kulaumiwa vikali,” aliandika ujumbe katika mtandao wa Twitter. “Nahurumia nchi yetu.”
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments