Dozen Afunguka Kuondoka Clouds Kama Ruge Angekuwa Hai | ZamotoHabari.



Hamis Mandi  (B Dozen) ameweka wazi kuwa kama aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi wa kituo cha habari cha Clouds Fm, Ruge Mutahaba angekuwa hai asingeondoka kwenye kituo hicho.

Akizungumza kwenye kipindi cha Gerezani kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ETV na kudai kuwa mapenzi yake kwenye tasnia ya burudani ndio yamefanya ahame kutoka clouds Fm na kujiunga na Efm.

“Nafikiri kama angekuwepo nisingeondoka Clouds, lakini mimi ni mtu ninayependa zaidi burudani kuliko kutangaza kwa hiyo Majizzo alivyonipa mipango yake nikaona huku ndiko kuna   Future” amesema Hamis.

Dozen alitambulishwa rasmi kwenye kituo cha E fm mapema Mwezi wa Juni baada ya kudumu clouds Fm kwa takribani miaka 9.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini