MSANII wa vichekesho Bongo, Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ amesema hana wivu hata kidogo na wasichana wanaochipukia katika uchekeshaji kwa sababu na yeye alitokea huko.
Akizungumza na AMANI msanii huyo alieleza kwamba kila siku vipaji vipya vinatokea hivyo anachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha anazidi kuwa bora katika sanaa hiyo na sio kuwaonea wivu.
“Unajua sasa hivi kuna wasanii wengi wa kike ambao wanafanya komedi tena wapo vizuri, sasa siwezi kusema nawaonea wivu nitakuwa sina akili, lakini ninachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuhakikisha naongeza ubora kwenye kazi zangu ili nisishuke kisanaa,”
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments