Mambo Matano Kuhusu Shangazi Fatma Karume | ZamotoHabari.


Kupitia kipindi cha SalamaNa inarushwa na East Africa TV kila Alhamisi kuanzia 3:00 usiku, Mwanasheria na Wakili wa kujitegemea Fatma Karume "Shangazi" amefunguka mambo mengi yanayomuhusu kuanzia siasa, sheria, familia, kazi na mahusiano.

Sasa haya hapa ni mambo matano ambayo ameweza kuyasema wakati anafanyiwa mahojiano na mtangazaji Salama Jabir "Ece Jay".

Kuvaa nguo nyeupe

Fatma Karume amesema ukiweka ahadi lazima utimize hivyo yeye ameweka nadhiri ya kuwa ataendelea kuvaa nguo nyeupe mpaka siku ya kupiga kura na hapendi kutofautishwa na wengine.

Vitu anavyopenda kuvifanya nje ya kazi zake

“Mimi Naweza kushona nguo zangu mwenyewe kwa kutumia Cherehani na najifunzia kwenye YouTube, napika udi mzuri, jam, nasoma sana hasa muda wa sasa na kazi yangu ya sheria inanifanya kusoma sana” amesema Fatma Karume

Kadi ya uanachama 

Fatma Karume amesema hana kadi ya chama chochote pia hajawahi kuomba wala kusaini kutaka kuwa na chama chochote, pia ameongeza kusema ni uhuru wake kutaka kuwa na chama au la.

Kifo cha Babu yake Mzee Abeid Amani Karume

Kwenye familia yao wamezaliwa watoto 6 na yeye ndiyo mtoto wa kwanza kuzaliwa, kuhusu kifo cha Babu yake Mzee Abeid Amani Karume amesema alikuwa na miaka mitatu, na anaikumbuka hiyo siku lakini hakuwa na fikra za kuelewa wakubwa wanachofikiria.

Ofisi yake kupigwa Bomu 

Moja kati ya tukio baya lililomtokea ni ofisi yake kupigwa bomu mida ya saa 8 usiku mwezi August 2017 na mpaka leo hajapewa ripoti ya polisi nani aliyefanya tukio hilo.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini