Mwaisa Nyonyoma, Fundi wa Kuchezesha Paka na Nyani | ZamotoHabari.


Kutana na Mwaisa Mzee wa Nyonyoma, Mnyakyusa wa kwanza ambaye ni mchekeshaji aliyejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamii ambapo anawatumiwa wanyama kama Nyani, Ngedere, Paka na Ngombe ili kuwaburudisha mashabiki zake.


Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Mzee wa Nyonyoma amesema alipata idea ya kutumia wanyama hao kwenye vichekesho mwaka 2017 ila alikuja kufahamika zaidi Novemba 2019.

"Sababu za kutumia Nyani ni kutokana na matukio yao yanaendana na binadamu kama sisi, kwa hiyo ninachofanya ni kutafuta ujumbe kupitia wale wanayama japo wapo wengine ambao nawatumia nje ya nyani na paka, pia video zile za wanyama wanavyofanya vitendo vyao nazitoa mtandaoni huwa nafikiria idea binafsi au vitu vinavyotrend" - Mwaisa Mzee wa Nyonyoma

Kwa urefu zaidi tazama hapa chini


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini