UONGOZI wa Simba umesema kuwa utawakera wapinzani wao wote ndani ya msimu wa 2020/21 kwa kuwa ina kikosi imara na chenye wachezaji bora katika kila sekta.
Simba imesajili nyota wapya saba ambao iliwatambulisha Agosti 22, Uwanja wa Mkapa kwenye kilele cha Simba Day ikiwa ni pamoja na Bernard Morrison, Charles Ilanfya, Chris Mugalu, Larry Bwalya, Joash Onyango, Ibrahim Ame na David Kameta.
Akizungumza na Championi Jumamosi,Ofi sa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa wata-wakera wapinzani wao bila kuchoka ikiwa ni pamoja na watani zao Yanga kwa kuwa wana kikosi kipana ambacho kinawapa nguvu ya kutamba ndani ya uwanja.
“Nakwambia tutawakera watu ndani ya uwanja kwa kuwa benchi la ufundi litakuwa na kazi ya kuchagua wanataka kianze kikosi kipi cha Larry Bwalya ambacho ndani yupo Bernard Morrison ama cha Chris Mugalu na ndani yumo Clatous Chama.
“Kwa namna ambavyo wachezaji wetu walivyo hasa falsafa ya Simba kucheza mpira mwingi wa pasi, acha tu msimu uanze tutashuhudia mengi kweli, hao wenzetu tutakutana nao tu,” alisema Manara.
STORI: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es salaam
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments