Mwanamke Mwenye Ndevu Kama za Mwanaume Afunguka "Niliwahi Hadi Kujipaka Kinyesi cha Kobe" | ZamotoHabari.

Pichani Queen Okafor mrembo huyo mwenye ndevu akizungumza katika interview mpya na gazeti la The Sun la Nigeria, amesema baadhi ya watu hudhani yeye ni mwanaume au hudhani ana jinsia mbili lakini kiuhalisia yeye amezaliwa mwanamke isipokuwa ndevu zilizomuota akiwa na miaka 21-22 ndio zimempa muonekano tofauti

Amesema alijaribu kuzitoa nywele ikiwemo kujipaka usoni kinyesi cha kobe kama baadhi walivyomwambia yanazuia nywele kuota ila kwake haikufua dafu. amesema utotoni hakuwa tofauti sana na wasichana wenzie. ameongeza kuwa hospitali wamemwambia hana tatizo lolote katika mfumo wake wa uzazi hasa ovary kuwa labda ilisababisha tatizo isipokuwa mama yake mzazi amemwambia tatizo hilo amelirithi upande wa familia ya mama yake

Ameongeza kuwa hapendelei kuvaa nguo nzito au zinazomfunika mwili sana akidai inamletea shida kubwa kutokanana na nywele alizonazo mwili mzima nguo zinalowa kwa jasho haraka na sehemu yenye joto hali huwa mbaya zaidi ingawa anasema hazimuumi ila kunakuwa inconveniences au kukosa comfortability

Changamoto nyingine amesema ni baadhi ya wanawake na wanaume wanaopenda mapenzi ndivyo sivyo kumfuata wakidhani ni mwenzao lakini anakataa kwakuwa hisia zake zinapenda mahusiano ya kawaida na mwanaume kama wanawake wengine na anashukuru tayari amepata mwanaume aliyemkubali na ndevu alizonazo

Amesema kudhuhakiwa na baadhi ya watu mwanzoni kulimnyima furaha na kukosa kujiamini lakini mchungaji mmoja alimwambia ajikubali ndivyo alivyoumbwa itampa amani. amesema siku moja akiwa ameenda harusini mwanamke mmoja mtu mzima alimfuata akamwambia usijihisi mnyonge ishi kwa furaha wewe pia yupo mwanaume kwa ajili yako utakuja kuolewa. mama huyo alimwambia hata binti yake ana ndevu nyingi lakini ameolewa nchini Holland na tayari yeye na mumewe wamezaa watoto. amesema hiyo ilimpa kujiamini na kuanza kujikubali tofauti na mwanzo

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini