Binti mdogo mwenye umri wa miaka minne tu, yupo Uwanja wa Ndege wa Kigoma, Magharibi mwa Tanzania. Pembeni yake, yupo bibi yake, akiwa amemshika mkono. Kwa pamoja, wanaitazama ndege ndogo iliyokuwa inaruka uwanjani hapo kuelekea jijini Dar es Salaam.
Ndani ya ndege hiyo, wapo wazazi wa binti huyu mdogo, pamoja na wadogo zake. Moyo wake umejawa na huzuni kwa sababu wazazi wake wanaondoka na kumuacha, anatamani kulia lakini sauti inasikika ndani ya nafsi yake.
“Wamekuacha kwa sababu hujui kuendesha ndege! Unatakiwa kujifunza kuendesha ndege ili siku nyingine wasikuache tena!” Haya ni makala ya Suzan Mashibe, mwanamke wa kwanza Mtanzania kupata leseni ya urubani nchini Marekani na kupiga picha na Rais George W Bush kwa kupongezwa
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments