Mwimbaji R. Kelly Ashushiwa Kipigo Cha Nguvu na Mfungwa Mwenzake | ZamotoHabari.

Mwimbaji R. Kelly ameripotiwa kupigwa na mfungwa mwenzake wakiwa gerezani. Taarifa kutoka mtandao wa TMZ zimeripoti kwamba mfungwa mmoja aliingia kwenye chumba cha Kellz na kuanza kumshushia kipigo kizito.

Hii inadaiwa kuchochewa na maandamano ya wafuasi wa Kellz ambayo yanaendelea nje ya gereza hilo la Metropolitan mjini Chicago. Maandamano hayo yanadaiwa kuwakera wafungwa wengine kwani wamekuwa wakifungiwa ndani kutokana na sababu za kiusalama.

Kipigo hicho kimetajwa kudumu kwa dakika chache na kwa sasa anapokea matibabu toka kwa madaktari ambaye amesema hajaumia kwa kiasi kikubwa au kuvunjika mfupa wowote.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini