Afya ya figo ni muhimu kama ilivyo afya ya moyo, hii ni kwa sababu figo ni moja ya kiungo ambacho husaidia kuchuja sumu mbalimbali ndani ya mwili na baadaye kutoa taka mwili kwa njia ya haja ndogo (mkojo)
Matatizo ya figo huweza kuchangia ugumu wa upatikanaji wa haja ndogo (mkojo) au miguu na mikono kuvimba.
Pia mtu mwenye shida ya figo huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo ya moyo.
Ulaji unaofaa mara zote husaidia sana kulinda afya ya viungo vyote muhimu ndani ya mwili ikiwa ni pamoja na figo na kuifanya iweze kufanya kazi zake vizuri ndani ya mwili.
Hata hivyo, kuna baadhi ya vyakula ambavyo tunaweza kusema ni vyakula rafiki kwa afya ya figo ndani ya mwili ni vyema ukafahamu hapa leo. Karibu>>>
Kabeji, hii ni mboga ambayo wengi wetu tunaifahamu sana na tumekuwa tukiitumia katika maisha yetu ya kila siku, lakini ni vyema msomaji wangu ukatambua kwamba mboga hii nayo inauwezo mzuri wa kulinda afya ya figo yako.
Samaki pia ni muhimu sana kwa afya ya figo, hii ni kwa sababu kitoweo hiki kina kirutubisho kiitwacho omega 3 ambayo huwa na nafasi nzuri ya kulinda afya ya figo, lakini pia samaki ni chanzo kizuri cha protini ndani ya mwili.
Pamoja na hayo, mafuta ya mzaituni nayo ni mazuri sana kwa kuboresha afya ya figo na kuikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Mafuta haya ya mzaituni ndani yake yana virutubisho mbalimbali kama 'oleic acid', anti-inflammatory fatty acids ambavyo vyote kwa pamoja hutetea afya ya figo ndani ya mwili, halikadhalika mafuta haya ni mazuri pia kwa afya ya moyo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments