STAA wa fi lamu za Kibongo, Shamsa Ford na mzazi mwenza wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Elibariki Emmanuel ‘Nay wa Mitego’; Siwema Edson, wameunda ushoga pambe pamoja na kwamba, wote walishatoka kimapenzi na jamaa huyo.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Siwema amesema kuwa, Shamsa amemlelea mtoto wake kwa mapenzi makubwa, hivyo hana tatizo naye. Siwema amesema tangu huko nyuma, hakuwa na chuki na Shamsa na ndiyo maana ametoka Mwanza hadi Dar kwenda kumuona shoga’ke huyo.
“Unajua ukimuona mwanamke mwenzako anamlea mtoto wako kwa mapenzi makubwa kama alivyofanya Shamsa, basi fahamu fi ka hata kama utatangulia mbele ya haki, mtoto wako ataishi maisha yasiyo na shida kabisa na ndiyo maana ninamheshimu sana Shamsa,” amesema Siwema.
Siwema na Nay walizaa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Curtis, lakini walitengana wakati mtoto huyo akiwa na umri wa miezi sita tu, hivyo Nay alibaki na mtoto akisaidiwa kulelewa na mama mzazi na Shamsa aliyekuja kuwa mpenzi wa jamaa huyo kabla ya kutengana.
STORI: IMELDA MTEMA, DAR
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments