Pichani:Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof Siza Tumbo (kushoto) akipokea pembejeo kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA), Vianey Rweyendela kwenye hafla iliyofanyika Kijiji cha Chala, wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa juzi. AGRA
walikabidhi zana mbalimabli za kilimo na maghala 25 yaliyokarabatiwa na ruzuku kutoka shirika hilo kwa ajili ya wakulima wadogo wa mkoa wa Rukwa na Katavi.
===== ======= =========
WADAU wa maendeleo ya Kilimo nchini wameendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza mpango wa maenmdeleo ya Kilimo wa pili (ASDP II).Lengo la ushirikiano huo ni kuhakikisha kwamba Kilimo kinachoendeshwa nchini Tanzania kinakuwa Kilimo biashara.
Hivi karibuni Shirika la Mapinduzi ya Kijani barani Afrika (AGRA) lilikabidhi miradi kadhaa kwa wananchi kupitia wizara ya Kilimo, iliyokarabatiwa na kujengwa kwa ruzuku ya shirika hilo mkoani Rukwa na Katavi. Miongoni mwa miradi hiyo ni maghala na pia mizani.
Miradi hiyo ilikabidhiwa kwa Naibu Katibu Mkuu Kilimo Prof Siza Tumbo na Mwakilishi mkazi wa AGRA nchini Tanzania Vianey Rweyendela. Kwa mujibu wa Prof. Tumbo katika utekelezaji wa mpango wa ASDP II serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba kila mkoa unazalisha ziada ambayo itaingia sokoni na kusifu mchango wa Agra katika kufanikisha hilo.
Miradi hiyo iliyokabidhiwa imo katika mradi mkubwa wa kuleta tija wa Agricultural Transformation in Africa (PIATA) ambao hapa nchini unaitwa PIATA-TIJA . Kwa kipindi cha miaka mitatu AGRA kupitia PIATA-TIJA imewafikia wakulima wadogo 127,000 na kuwawezesha kuongeza uwezo wao wa kuzalisha kwa kuangalia halia ya soko hukuw akipunguza maumivu ya bei kwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi mazao yao.
Mazao ambayo yapo katika mpango huo ni mahindi, maharagwe na mpunga.
Washiriki katika PIATA-TIJA ni Bill & Melinda Gates Foundation (BMGF); Rockefeller Foundation (RF); United States Agency for International Development (USAID), Department for
International Development (DFID), na German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ).
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments