WASHINDI WATUNUKIWA TUZO MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KATI DODOMA | ZamotoHabari.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akimkabidhi Mkaguzi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Makao Makuu, Kanali Philip Mahende Kombe la Ushindi wa Jumla wa Maonesho ya Nanenane, Dodoma. Kanali Mahende alimwakilisha Mkuu wa JKT Tanzania. Maonesho hayo ya Kanda ya Kati yanajumuisha wakulima, wafugaji wavuvi na Taasisi mbalimbali za mikoa ya Singida na Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akiwakabidhi wawakilishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kombe la Ushindi wa Pili wa Jumla wa Maonesho ya Nanenane ya Kanda ya Kati jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma, ACP Keneth Mwambije Kombe la Ushindi la ushindi wa tatu wa Jumla wa Maonesho ya Nanenane, Dodoma. ACP Mwambije alimwakilisha Kamishna Mkuu wa Magereza Tganzania.

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stelah Ikupa akikabidhi cheti na Kombe kwa wawakilishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambayo imepata ushindi wa kwanza wa Paredi ya Wanyama.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Mkaa Mweupe, Aristotre Nikitas akipokea cheti ushindi wa pili wa kundi la Wajasiriamali na Wawekezaji Wadogo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stelah Ikupa .

Julius Soniga akikabidhiwa cheti cha ushindi wa tatu katika kundi la Ufugaji Bora katika maonesho hayo.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stelah Ikupa akimpongeza Kiongozi Msanii wa Kikundi cha Ngoma cha Mwinamila kiichotumbuiza maonesho hayo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stelah Ikupa akihutubia katika hafla za kunga rasmi maonesho hayo

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga (kushoto) na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo,Zahara Michuzi wakifurahia Mkulima kutoka wilaya hiyo, kupata cheti cha ushindi wa Mkulima Bora katika Maonesho hayo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Steah Ikupa akiwakabidhi maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii, cheti cha ushindi wa kwanza kundi la Wizara Sekta ya Uchumi Uzalishaji katika maonesho hayo yaliyofikia kilele leo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara hiyo. Doreen Makaya.

Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Steah Ikupa akikabidhi cheti cha ushindi wa tatu wa Bodi za Mazao na Mifugo kwa mwakilishi wa Bodi ya Mtama.

Wakuu wa Wilaya za mikoa ya Dodoma na Singida wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhudhuria kufungwa rasmi kwa Maonesho ya Wakulima ya Nanenane ya Kanda ya Kati, yaliyofungwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulmavu), Stelah Ikupa kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.






Wananchi wakiwa wamesongamana kugombea kuingia kwenye viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati vilivyopo Nzuguni, jijini Dodoma. Kiingilio kilikuwa sh. 1000 kwa wakubwa na watoto sh. 500. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-CCM BLOG


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini