Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akipokea Mfuko wa Mbegu Mchanganyiko ktuoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha World Vegetable Center Dr Gabriel Rgelema (Aliyevaa Shati la Bluu)alipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Nyakabidi Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akipata maelezo jinsi Wadudu waharibifu wa mazao ya mbogamboga wanavyoweza kukabiliwa kwa njia ya asili ktuoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha World Vegetable Center Dr Gabriel Rugelema (Aliyevaa Shati la Bluu)alipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Nyakabidi Mkoani Simiyu.
Na.Vero Ignatus.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa amewataka wakulima wa Mboga mboga kuchangamkia Mikopo inayotolewa na taasisi za Kifedha ili kuinua hali ya Uzalishaji Mazao na kujiongezea kipato kupitia kilimo cha Bustani.
Waziri Mkuu Mjaliwa maeyasema hayo Mkoani Simiyu katika kilele cha maonesho ya nane nane huku akizipongeza baadhi ya sekta binafsi ikiwemo TAHA kwa kujikita katika kutoa mafunzo kwa wakulima wa bustani.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema Wizara yake imezunguka Nchi nzima na kufanikiwa kupunguza Migogoro ya Wakulima na wafugaji hali ambayo wizara hiyo inajivunia.
Aidha Waziri Mpina amesema katia upande wa chanjo na uhilishaji serikali imeweka bei elekezi ya uhimilishaji ambapo kwa sasa Ng’ombe mmoja atagharimu kiasi cha 10,000 badala ya sh.25,000 ambapo katika maonesho ya nane nane msimu huu Wizara hiyo imeweza kuhimilisha Ng’ombe zaidi ya 100 bure .
Naye Waziri wa Kilimo Japheti Hasunga amesema kwa sasa Wizara ya kilimo imejikita kuhamaisha wakulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuhamia katika kilimo cha Biashara na tayari Wizara hiyo imeanzisha huduma za ugani ambazo zitatolewa huku Jengo la Wizara ya kilimo lililopo ndani ya Viwanja vya Nyakabindi likipangwa kutumika kutoa mafunzo mwaka mzima,ambapo amaewaomba viongozi wa Mikoa husika kuhakikisha wanaleta wakulima ili wapate mafunzo.
Miongoni mwa wadau walioshiriki Maonesho hayo ni kituo cha Kimataifa cha Utafiti cha World Vegetable Cenenter Mkurugenzi wa kanda ya Mashariki na kusini mwa bara la Afrika ke Dr Gabriel Rugelema amesema maenosho hayo yametoa taswira jinsi jamii ilivyo na uelewa juu ya kilimo cha asili nakubaini kuwa baadhi yao wako nyuma hivyo taasisi hiyo inakwenda kujpanga ili kuifikia Jamii nakutoa Mafunzo kwa Wakulima hao.
Dr Rugelema ameongea kuwa Msimu huu wameleta pia viuongo vya Mboga vya asili hali ambayo itawasukuma kuongeza ukubwa wa benki ya Mbegu na kuzisambaza kwa wakulima (Seed Kit) huku akiahidi kuweka Ofisi katika Jengo la kilimo liliopo katika Viwanja vya Nyakabindi.
Kilele cha Maonesho ya nane nane kimetamatika tarehe 8,ambapo kitaifa Mwaka huu yamefanyika Mkoani Simiyu na kauli mbiu ikisema kwa Maendeleo ya kilimo,Uvuvi na Ufugaji tuchague Viongozi bora 2020.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments