Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv.
Watu wasiofahamika na wenye Nia mbaya wameendelea na vitendo Vya uchomaji Moto ovyo maeneo mbalimbali Mkoani Kagera, hali ambayo imeonekana kusababisha Hasara kubwa ya Mali ikiwemo mazao na miundo mbinu.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa Agosti 06, 2020 na kitengo Cha mawasiliano TANESCO Mkoa wa Kagera imeeleza kuwa, Kagera imekuwa miongoni mwa waathirika wa matukio hayo ambapo imeripotiwa Mara kadhaa Hasara kubwa ambayo imekuwa ikijitokeza kufuatia uchomaji Moto huo katika mbuga, mapori, na mashamba hivyo kupelekea taharuki kubwa na hofu kwa wakazi wa maeneo husika.
Licha ya Taarifa iliyotolewa wiki hii ya kushikiliwa kwa mtu mmoja Wilayani Biharamulo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo hivyo, vilivyosababisha kuingia kwa nguzo za umeme, Hali Kama hiyo imeonekana kujitokeza pia Wilayani Muleba ampapo Watu ambao bado hawajafahamika *wamewasha Moto uliosababisha kuungua kwa nguzo nne za kusafirisha umeme eneo la Gera Kashasha Wilayani Muleba.
Tukio hilo limesababisha baadhi ya Maeneo Wilayani Muleba kukosa huduma ya Umeme,Wakati wataalamu kutoka Shirika hilo na mafundi wakiendelea na kazi ya kurejesha huduma ya umeme, TANESCO kwa kushirikiana na vyombo vya usalama inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika.
Huku wito ukitolewa kwa Wananchi kushiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments