Katibu wa benki ya Stanbic Hellen Makanza (kushoto)) akiongea na Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Watoto Wetu Tanzania (WWT), Evans M. Tegete (watatu kushoto) wakati akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa madarasa katika kituo cha Watoto wetu Tanzania mjini Msata, Chalinze hivi karibuni. Jengo hilo linajengwa na benki hiyo kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta ya elimu Tanzania. Wengineo ni Meneja Uhusiano wa Wafanyakazi wa Stanbic Tanzania, Beatrice Monyo (aliyesimama mwenye T-shirt ya blue), Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Benki ya Stanbic, Bi Eutropia Vegula, (kulia) na Mratibu wa WWT, Moses Ngenzi (wapili kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Watoto Wetu Tanzania (WWT), Evans M. Tegete (watatu kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Stanbic baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa madarasa katika kituo cha Watoto wetu Tanzania mjini Msata, Chalinze hivi karibuni. Jengo hilo linajengwa na benki hiyo kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta ya elimu Tanzania. Wengineo ni Meneja Uhusiano wa Wafanyakazi wa Stanbic Tanzania, Beatrice Monyo (aliyesimama mwenye T-shirt ya blue), Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Benki ya Stanbic, Bi Eutropia Vegula, (kulia) na Mratibu wa WWT, Moses Ngenzi (wapili kulia) na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Benki ya Stanbic, Bi Eutropia Vegula, (kulia)
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments