WILAYA YA NYASA YAWAPIGA MSASA MAAFISA WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA | ZamotoHabari.



……………………………………………………………

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imeanza kutoa mafunzo ya siku
tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi Ngazi ya kata kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 28 Oktoba, 2020.

Mafuzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Cassim Majaliwa ulioko katika Shule ya Sekondari Mbambabay, Wilayani hapa, na yametolewa na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Nyasa Ndugu Jimson Mhagama ambaye pia Mkurugenzi Mtendaji wa Malmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Akifungua Mafunzo hayo Bw. Jimson Mhagama amewataka wasimamizi hao kujifunza na kuelewa vizuri, mafunzo kwa kuwa yanalengo la kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kujiamini, na kutekeleza ipasavyo majukumu ya Usimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata.

Bw Mhagama ameongeza kuwa washiriki wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi wameteuliwa kwa kuaminiwa kuwa wanauwezo, wa kusimamia majukumu haya ipasavyo, hivyo wanakila sababu ya kujituma, kujiamini, kwa kufuata Katiba ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Sheria ya Uchaguzi, Maadili na Maelekezo ya Tume ya Uchaguzi ili kuweza kusimamia uchaguzi katika Maeneo yao.

“Ndugu washiriki mafunzo haya ni ya muhimu sana kwa kuwa yana lengo la kutujengea uwezo wa kutekeleza majukumu yetu katika kipindi cha uchaguzi hivyo tunatakiwa kuwa makini, tuyasikilize na tukayafanyie kazi kwa lengo la kutekeleza majukumu yetu ipasavyo.

Aidha amewaagiza wasimamizi hao wa Uchaguzi ngazi ya Kata, kuvishirikisha vyama vya siasa na wadau wa Uchaguzi kwa kila jambo , wanalotakiwa kushirikishwa ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki. Pia aliwakumbusha wanatakiwa kuijua miundombinu yote katika maeneo yao na jinsi ya kuifikia kwa harak katika Vituo vyote vya kupigia kura ili watekeleze majukumu yao Vizuri.

Katika hatua nyingine Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata walipewa kiapo cha kutunza siri pamoja na Tamko la kujitoa uanachama wa chama cha siasa.

Hii ni kwa matakwa ya Kanuni ya 16(1)(a) na 50(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge,2020 na Kanuni ya 14(1)(a), na(2) na 43(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) ikisomwa pamoja na Kanuni ya 16(1)(b) na (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge,2020 na Kanuni 14(1)(b) na (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,(Uchaguzi wa Madiwani, 2020)


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini