Aliyekosa Uenyekiti ACT Wazalendo, kugombea Urais | ZamotoHabari.


Aliyewahi kuwania nafasi ya Uenyekiti Taifa kupitia Chama cha ACT Wazalendo Yeremia Kulwa Maganja, leo amepitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi, kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wajumbe wa Mkutano huo Mkuu wamempitisha jana Agosti 7, 2020, kwa kumpa kura 231 kati ya kura 258, ambapo kati ya hizo zilizoharibika ni kura 7 na kura za hapana ni 20.

Mara baada ya kutangazwa kupeperusha bendera ya chama hicho, Mayanja naye alimchagua mgombea mwenza ambaye ni Haji Ambari Hamis, aliyewahi kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi mwaka 2010.

Awali wagombea wa nafasi hiyo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi walikuwa ni watatu akiwemo Petterson Walter Mshenyella na Samweli Christopher Ruhuza, lakini baadaye walijitoa katika mchakato huo kwa kusema kuwa wameweka matamanio yao pembeni na kuangalia maslahi makubwa ya chama.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini