ALIYOSEMA MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI LEO SEPTEMBA 1, 2020 WILAYANI BAHI, MKOANI DODOMA WAKATI WA MKUTANO WA HADHARA
#Nawahakikishia wananchi wa Bahi kuwa sitawaangusha, nabaki na deni kwenu hivyo niwaombe muendelee kuniamini na kuchagua Chama cha Mapinduzi ili tuendeleze kazi tuliyoanza ya kuleta mageuzi.
#Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya umefikia asilimia 95 na unatekelezwa kwa gharama ya TZS bilioni 1.8.
#Hospitali ya Wilaya ikamilishwe haraka ili wananchi waanze kupata huduma hapa.
#Vituo vya afya vitatu vimejengwa kwa gharama ya TZS bilioni 1.5 katika maeneo ya Mdemu, Chifukuta na Bahi mjini.
#Nawapongeza wananchi wa Bahi kwa kuchapa kazi na kufanya uzalishaji katika sekta ya kilimo.
#TZS bilioni 2.1 zimetumika kugharamia elimu bila malipo katika Wilaya ya Bahi.
#Shule mpya 3 zimejengwa na madarasa 51.
#Vijiji 11 vimenufaika na mradi wa visima ikiwa ni moja ya hatua za kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji.
#Vijiji 43 vya wilaya ya Bahi vimefikishiwa umeme na vilivyobaki vitafikishiwa huduma hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
#Katika kipindi cha miaka mitano ijayo tutawawezesha wananchi kupata huduma bora za ugani katika wilaya hii.
#TZS milioni 149 zimetolewa kwa vikundi vya akinamama, wanawake, vijana na walemavu ili kuwawezesha kujiajiri kupitia vikundi vyao.
#Katika kipindi cha miaka mitano ijayo tutaendelea kuimarisha huduma za afya, maji, elimu na miundombinu.
#Wilaya ya Bahi inafanya vizuri katika uzalishaji wa mpunga.
#Tulishapitisha sheria ya kuzuia wananchi kutozwa ushuru wanaposafirisha mazao yao yasiyozidi tani moja.
#Tozo 114 zimefutwa ili kuwasaidia wakulima na kuwaondolea usumbufu uliokuwepo awali.
Imeandaliwa na Mwandishi Maalum Dodoma

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments