Na Said Mwishehe,Bahi-Michuzi TV
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.John Magufuli amewahkikishia wananchi wa Wilaya ya Bahi kuwa wakimchgua katika Uchaguzi Mkuu mwaka unaotarajia kufanyika Oktoba 28 atahakikisha anaendelea kuleta maendeleo kwa kasi kubwa ikiwa pamoja na kumalizia viporo vilivyobaki.
Dk.Magufuli amesema hayo leo Septemba 1, 2020 wakati akizungunza na maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Bahi alipokuwa akiomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu na wingi wa wananchi amewaambia ana deni kubwa ya kuwapelekea maendeleo na kwamba hatawasahau.
Wakati anaanza kuzungumza Dk.Magufuli amesema katika kuleta mabadiliko ya kweli katika maeneo yetu katika mambo ya kitaifa tayari amezungumza juzi, ya kimkoa ameshazungumza na leo yuko Bahi ambako kuna niko mengi yamefanyika.Hata hizi nyumba huko nyuma haizikuwa hivyo.Mmepiga hatua kubwa ndani ya miaka mitano.
"Tumejenga Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya vitatu vya Bahi, Kifukuta na Mdemu.Nataka hospital imelizike haraka,ndio maana naomba mnipe kura nimalizie kiporo kilichobaki kwani imekamilika kwa asilimia 95
"Nimekuja kuomba kura nataka katika miaka mingine mitano elimu bure iendele.Hapa Bahi tumetumia Sh.bilioni 2.1 na tutaendelea kutoa elimu bure,ndio maana nimekuja kuomba kura kwenu.Katika miradi ya maji tumetumia Sh.bilioni 2.9 katika maeneo ya Magage, Bahi,Mkatike, Mdem na Ngugi. Pia kuna tumetekeleza miradi ya maji katika vijiji vya Zanka,Nondwa na Zegele na kuchimba visima vingine 11.Najua tatizo la maji bado lipo Bahi naomba mnibebeshe hii changamoto,tutaimaliza,"amesema Dk.Magufuli.
Kuhusu umeme, Dk.Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano vijiji 43 vimepata umeme kutoka vijiji vinne mwaka 2015 na kwamba kuna vijiji 16 ambavyo bado havijaunganishiwa umeme,hivyo anaomba kura ili amalizie vijiji hivyo.
Pa amewaambia wananchi hao kuwa wameendelea kujenga barabara na kwamba anataka akichaguliwa tena amalizie ujenzi wa barabara kwa fedha za ndani."Naombe mnipe nafasi nimalizie".
Kwa upande wa wakulima na wafugaji ,Dk.Magufuli amesema anatambua namna ambavyo wakulima wanafanya kazi nzuri katika kilimo na anatambua juhudi za wafugaji katika Wilaya hiyo,hivyo ameahidi kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo na mifugo.
"Nataka kuendelea kusaidia wafugaji, watu Bahi ni wafugaji wazuri,pia tutaendelea kusaidia wakulima wa Bahi.Tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuimarisha sekta ya kilimo,tumefuta tozo za kodi 114 .Kuhusu kusaidia kaya masikini hapa Bahi tumetumia Sh.bilioni tano kupitia mfuko wa TASAF,"amesema Dk.Magufuli na kuwasisitiza ikifika siku ya kupiga kura wampigie ili aendelee kuleta maendeleo ya wananchi wa Bahi.
Pamoja na hayo Dk.Magufuli amesema katika miaka mitano watendeleza pale walipoishia, wataendelea kujenga shule na madarasa,kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya barabara, kuweka umeme, kutoa elimu bure ,kuboresha aekta ya afya na sekta nyingine mbalimbali.
"Wingi wenu huu nimebaki na deni kubwa naombeni mnichague , muwachague madiwani wa CCM na mbunge wa CCM .Hata hivyo kwa sasa Serikali iko Dodoma,na mimi niko Dodoma, sitaisahau Bahi kwanza haiko mbali na Dodoma,nitaleta maendeleo.
"Mpeni kura mbunge wa hapa,tumechelewa sana, tupeni nafasi tutafanya kazi isiyo na mfano. Miaka mitano ya mwanzo ilikuwa onja onja tu na sasa tunakwenda kufanya kazi kweli kweli.Hata hivyo nchi yetu iko kwenye nafasi ya 10 katika maendeleo ya kiuchumi, nchi yetu katika usalama na kwa Afrika iko nafasi ya sita na kwa duniani iko nchi ya 52,"amesema Dk.Magufuli.

Mgombes Urais wa CCM, Dk John Magufuli akiwaaga wananchi na wanachama wa chama hicho wakati akiondoka kwenye kampeni zake Wilaya ya Bahi ambapo ameelekea wilayani Manyoni Singida.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments