CHAMA CHA SAU WAZINDUA KAMPENI ZA URAIS JIJINI DAR, WANADI SERA YA KILIMO NA VIWANDA | ZamotoHabari.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
CHAMA cha Sauti ya Umma (SAU) wamezindua kampeni za Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Muttamwega Bhatt Mgaywa katika eneo la kwa Zoo, kata ya Buyuni jimbo la Ukonga Wilaya ya Ilala na kunadi sera katika eneo la ukonga  jijini Dar es Salaam.

Katika Uzinduzi chama cha SAU wamezindua Ilani ya chama hicho pamoja na uzinduzi wa kilimo kwa kutumia Trekta huku akiwa na kuachana na kilimo cha mkono.

Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhandisi Muttamwega Bhatt Mgaywa amesema kuwa kwa sasa serikali ni lazima iwe ya kilimo na viwanda.

"Tunakwenda kutekeleza ilani ya chama cha Sauti ya Umma (SAU) tukishinda uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, 2020."

Amesema kuwa serikali ya Kilimo na Viwanda ndiyo itakayozalisha ajira nyingi na bora kwa watu wote.

Chama cha SAU kina vipaumbe vya Afya elimu na kilimo na viwanda. Huku wakiwa na sera ya Elimu bure kuanzia Chekechea hadi chuo kikuu afya bure kwa wote.

Katibu mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majaliwo Kyara amesema kuwa amesema kuwa Ilani ya chama cha SAU kitakwenda kuzalisha ajira zaidi ya milioni tisa katika miaka mitano kama wananchi watawapa ridha ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Hata hivyo amesema kuwa Ilani ya chama wakichaguliwa watabadilisha mitaala ya elimu kwani kunamasomo yanafundishwa hayasaidii katika maisa ya kawaida ya Mtanzania.

"Ilani ya chama chetu imeeleza kubadili mitaaala ya elimu watu wanakaa wanasoma vitu vingi ambavyo baadae katika maisha hawavitumii na Ilani hii imejikita zaidi katika kumkomboa mkulima ambao ni wengi katika nchi hii." Amesema Kyara

Kwa upande wa walemavu  ilani ya chama hicho imejikita kuwasaidia walemavu kwa kuwapa vifaa saidizi bure.

Ilani hii imejikita kuhakikisha kila mtanzania anafaidi matunda ya nchi yake ya Tanzania. Amesema Kyara. 

Kwa upande wake Mgombe Ubunge jimbo la Kibamba kupitia chama cha Sauti ya Umma (SAU), Kunje Ngombalemwilu amesema kuwa endapo wananchi wakiwapa ridhaa ya kuongoza nchi hii watajenga zahanati kila mkoa pamoja na kupeleka ndege kila mkoa kwaajili ya kusafirisha abiria.

Amesema katika Ilani ya Chama cha Sauti ya Umma hawapingi kila kitu lakini katika Ilani ya Chama hicho utekelezajimiradi watapunguza muda.

Hata hivyo katika uzinduzi wa kampeni hizo akiwa ameambatana na mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa chama hicho Satia Mussa Bebwa pamoja na Mgombea wa Urais wa Serikali ya Zanzibar, Issa Zonga.
Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Derpha Mpata akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ilani ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU) katika uzinduzi wa Kampeni za chama hicho zilizofanyika  kwa Zoo, kata ya Buyuni jimbo la Ukonga Wilaya ya Ilala na kunadi sera katika eneo la ukonga  jijini Dar es Salaam.
Mgombea Urais akiwa na mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa chama hicho Satia Mussa Bebwa pamoja na Mgombea wa Urais wa Serikali ya Zanzibar, Issa Zonga akiwa katika Trekta wakati wakizungua kilimo kwa kutumia Trekta.
mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa chama hicho Satia Mussa Bebwa akizungumza na wananchi wa Kwa Zoo wakati wa kuzindua kampeni za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Sauti ya Umma (SAU).
Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhandisi Muttamwega Bhatt Mgaywa  wa kwanza ktoka kushoto  akiwa na mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa chama hicho Satia Mussa Bebwa pamoja na Mgombea wa Urais wa Serikali ya Zanzibar, Issa Zonga wakichimba viazi mara baada ya kuzindua Kilimo kwa kutumia Trekta na Kuachana na Kilimo cha Mkono.
Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhandisi Muttamwega Bhatt Mgaywa  akizungumza akiwa shambani mara baada ya kuzindua kampeni za chama cha SAU.
Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhandisi Muttamwega Bhatt Mgaywa  akiwa na mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa chama hicho Satia Mussa Bebwa pamoja na Mgombea wa Urais wa Serikali ya Zanzibar, Issa Zonga wakiwa wamebeba matufali kuashiria kujienga nyumba za kisasa kwa kila mtanzania.
Viongozi mbalimali wa chama cha Sauti ya Umma wakiwa katika Kampeni za Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.
Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhandisi Muttamwega Bhatt Mgaywa aliyebemba miwa.
Mgombe wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhandisi Muttamwega Bhatt Mgaywa akionesha kiazi alichochimba shambani.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini