KATIBU MKUU DK.ALOYCE NZUKI AWAPONGEZA SAO HILL KUVUKA LENGO UKUSANYAJI WA MAPATO. | ZamotoHabari.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Aloyce Nzuki akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.



Na Fredy Mgunda,Mufindi.


Katibu mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii amewapongeza TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa kuvuka lengo la makusanya ya mapato ya mwaka.

Akizungu alipokuwa alipotembelea Shamba la Miti Sao Hill,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Aloyce Nzuki alisemakuwa ameona shughuli za upandaji miti za utunzaji zinazofanywa na shamba
.
Alisema kuwa anatoa pongezi hizo kwaTFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill kwa kufaya kazi nzuri ambayo hupelekeataifa kunufaika kutokana na uwepo wa Shamba hili ambalo ni shamba kongwe nashamba kubwa kuliko mashamba yote ya miti ya kupandwa nchini.

"Mnafanya kazi nzurisana,nimeona hapa kwenye taarifa yenu ,wakati wengine wamepata shida sanakipindi cha Covid lakini ninyi mmeweza kufanya biashara vizuri, nikiangaliajedwali ambalo Mhifadhi Mkuu amelisoma jedwali namba tatu,naona hapa kwaujumla miaka hiyo mitano iliyotajwa mmevuka lengo kwa asilimia kumi na mbili(12%) ambayo ni mafanikio mazuri sana"Alisema Dr. Aloyce Nzuki

"Lakini kwa mwaka ule 2018/2019tayari mlikuwa mmeshavuka lengo kwa asilimia 28.7 (28.7) mlikuwa mko juu yamapato yale ya nyuma yake,na mmeonesha mnauwezo mkubwa sana wa kufanya biasharayote inayohusiana na mazao ya misitu lakini pia ya mazao ya nyuki",Alisema
Dr Nzuki

Aliendelea kusema kuwa kwa jitihadahizo TFS inastahili kupongezwa na kuwataka kuendelea kuhamasishanawatumishi wote kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza pato la taifa.

Aliwaeleza watumishi kuwa utekelezajiwa Ilani unategemea sana jitihada za watumishi walio na weredi,kujituma nauzalendo na hivyo eneo ambalo TFS inalisimamia ni maeneo ambayo yameelekezwa naviongozi ili kuchangia ukuaji wa pato la taifa.

"Niseme kitu kimoja majukumuambayo yapo mbele yetu ni kutokana na ilani ya Chama cha Mapinduzi kwambaeneo hili ambalo mnalisimamia ambalo linatokana mazao ya misitu na nyuki ni maeneo ambayo yametajwa na yameelekezwa na ilani yanayotarajiwa kuchangia kwakiasi kikubwa katika maendeleo ya taifa na mwananchi mmojammoja,”Dr Nzuki

Hata hivyo aliitaka TFS kupitiaShamba la Miti Sao Hill kuendelea kuweka ushirikiano mkubwa na jamiiinayolizunguka shamba ili kuepuka majanga ambayo yanahatarisha usalama washamba na mali zilizomo ambayo yamekuwa yakijitokeza


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini