MGOMBEA WA CCM EXAUD KIGAHE ATAJA VIPAUMBELE NANE VYA MAENDELEO JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI | ZamotoHabari.


Mgombea ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe akiomba kura kutoka wanachi wa jimbo hilo

Mamia ya wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kamapeni za mgombea ubunge wa Jimbo hilo.




Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazinikupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe ametoa ahadi za nane kwawananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamapeni zakuomba kura kwa wananchi wa jimbo la Mufindi,Exaud Kigahe alisema kuwa jimbo laMufindi Kaskazini linakabiriwa na changamoto ya miundombinu ya Barabara ambazozimekuwa hazipitiki kwa msimu mzima hivyo akipewa ridhaa ya kuwa mbungeatahakikisha anatatua kero hiyo.

Alisema kuwa atahakikisha anaboresha sekta yaElimu kwa kujenga na kukarabati majengo ya shule,kuanzisha mashindano ya kumpata mwananfunzi bora namwalimu bora kwa atakayefanya kazi nzuri ya kuwasaidia wanafunzi kufaulu kwawastani mzuri.

“Wananchi wa jimbo la Mufindi wengi niwakulima hivyo siwezi kuisahau sekta ya kilimo kwa kuwa hata mimi nimekuliakwenye family ya wakulima hivyo nitahakikisha kuwa tunaboresha masoko ya wakuliwa ili waweze kuuza mazao yao kwa bei nzuri” alisema Kigahe

Aidha Kigahe alisema kuwa ahadi nyingine ni pamoja na viwanda,afya,biashara,umeme na michezo ambazo atazifanyia kazi kama akiwambunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

“Kazi kubwa mliyonipa nitaifanya kwa nguvu naniwahakikishie sisi wabunge watatu wa Wilaya ya Mufindi (Kihenzile na Chumi)tutafanya kazi kwa pamoja kwa kuwa lengokubwa ni kuleta maendeleo”alisema Kigahe

Lakini pia Mgombea Ubunge Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi
Ameshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Mufindi Kusini na Kuwaomba Wananchi kuhakikisha Wanampa kura Za Kishindo Mh Rais, mbunge,Madiwani wote waCCM.

Naye Katibu Wa CCM Wilaya ya Mufindi Mgego amewahakikishia Kuwa
chama cha mapinduzi kitapata ushindi wa Kishindo hivyo wanaCCM wanatakiwa kuwa
mstari wa Mbele kutafuta kura za Mh Rais,Wabunge na Madiwani wa CCM.

Kwa upende wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Dr Abel Nyamahanga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wakampeni hizo aliwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuhakikishawanampa kura nyingi Mgombea Ubunge Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe kwa kuwaameamini na Rais.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini