KUTOZINGATIA ELIMU YA USALAMA MAKAZINI HUSABABISHA CHANGAMOTO ZA AJALI | ZamotoHabari.


NA DENIS MLOWE,KIHANSI

LICHA ya kuwepo kwa sheria na Mafunzo yanayohusu afya na usalama Kazini,lakini bado inaelezwa kuwa watu wengi hufa na kujeruhiwa kazini kwa kushindwa kuzingatia elimu wanayoipata Hivyo ni wazi kwamba sheria pekee haziwezi kuleta usalama kazini waajiriwa wanalo jukumu la kujilinda na kuwalinda wengine.

Akitoa Taarifa juu ya hali ya Afya na Usalama kazini,Meneja wa kitengo cha Afya Usalama Kazini wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mhandisi Fredy Kayega wakati wa hafla ya Kukabidhi Vikombe  kwa washindi wa Shindano la 10 katika siku ya Afya na Usalama kazini iliyoandaliwa na Shirika hilo alisema jitihada zinaendelea kufanywa na shirika katika kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa salama ili waweze kufanya kazi na kuhudumia wananchi kwa usalama zaidi.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo shirika la Tanesco liliamua kuanzisha Mashindano ya Siku ya Afya na Usalama Kazini ili kuhamasisha Vituo na Mikoa inayozalisha Umeme kuzingatia suala hilo kwa Manufaa ya Taifa na wafanyakazi kwa ujumla.

Alisema kuwa Msingi wa Maadhimisho ya Afya na Usalama kazini katika Shirika letu ni kuinua  uelewa na kutekeleza adhma hiyo kwa vitendo ili kupunguza changamoto ya Ajali zinazotokea katika maeneo ya kazi kwa kufanya hivyo Shirika litaondokana na Madhara kwa wafanyakazi kwa shughuli zinazofanywa katika kuwaletea wananchi huduma.

Alisema Mashindano hayo yamekuwa yakisaidia kupunguza athari zinazojitokeza kwa wafanyakazi wawapo kazini kwa kuongeza Umakini katika maeneo yao ya kazi tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kwa Mujibu wa Utafiti Uliofanywa na Idara ya Afya na Usalama kazini imeonesha kutokuwa na  uelewa wa wafanyakazi ambapo katika kipindi cha mwaka 2016 uelewa ulipanda hadi asilimi 76%,2017 asilimia 78%, na Mwaka 2018 ni asilimia 79% na 2019 uelewa ulifika asilimia 80% hali inayoashiria itasaidia kupunguza madhara yanyoweza kujitokeza.

“Pamoja na jitihada hizi na tathimini hizi zinazofanyika lakini kuna changamoto kubwa inaambatana nazo ikiwemo ajali zinazowakabili wafanyakazi kwa mfano mwaka 2017/2018 matukio ya Ajali na ndani ya Shirika zilikuwa 58,na kwa mwaka 2018/2019 ajali zilishuka hadi kufikia Ajali 50 lakini changamoto ikawa kubwa katika kipindi cha mwaka 2019/2020 ajali kazini zikapanda hadi kufikia 80 zikisababishwa na Magari kwahiyo changamoto hizi zinatufanya tuendelee na juhudi kuhakikisha tunakuwa salama”Alisema

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi Raslimali watu wa Tanesco, Francis Sanguna  akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO  alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Afya na Usalama kazini Shirika lilitengeneza Sera ya Afya na Usalama kazini mwaka 2008 lengo ikiwa ni kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa salama wawapo kazini na nje ya kazi ambapo elimu imekuwa ikitolewa ili kufikia lengo la Ajali sifuri.

Aidha amewaonya wale watakaokiuka Misingi ya Afya na Usalama Kazini kuwa sheria kuwa Shirika la Umeme Tanzania halitamvumilia Mfanyakazi yeyote atakayehatyarisha Usalama kwanamna yoyote ile kwani kwa kufanya hivyo kutachangia kuongeza nidhamu kwa wafanyakazi.

“Niwaonye wafanyakazi wa TANESCO Shirika halitasita kumchukulia hatua yeyote atakayeshindwa kuzingatia Sheria za Afya na Usalama Kazini na kusababisha madhara kwa wengine hivyo kila mmoja azingatie kuwa Afya na Usalama kazini ndiyo msingi wa Maendeleo ya Taifa”alisema

Nao Levocatus Meshack ni Meneja wa Kituo cha Uzalishaji Umeme cha Kihansi na Clement Mwakalosi ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Shirika hilo walieleza namna hatua zinavyochukuliwa kwa kuhakikisha Huduma za Umeme zinaendelea kutolewa kwa kuzingatia Afya na Usalama kazini na kuleta Maendeleo Nchini kwani juhudi kubwa ni utoaji wa elimu jambo lililowafanya kuwa washindi wa Kwanza katika shindano hilo kwa Upanbde wa Vituo vya Kuzalisha Umeme.

Washindi katika shindano hilo ambalo ilibidi lifanyike mwaka huu mapema liliarishwa kutokana na ugonjwa wa Covid 19  kwa Mwaka 2018/2019 kwa upande wa Vituo vya Kuzalisha Umeme na Kwa Upande wa Mikoa Mkoa wa Katavi ndiyo ulifanikiwa kushinda ukifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma na Mshindi wa Tatu ambao ni Mkoa wa Kinondoni Kusini na kituo cha Kidatu ambao ndiyo waliokabidhiwa vikombe.
Meneja Raslimali Watu (kushoto) Mhandisi Francis Sangunaa akikabidhi mmoja wa washindi wa Mikoa Kombe baada ya kufanya vizuri katikaIsimamizi wa  masuala ya Afya na Usalama Kazini
Baadhi ya Washindi wa Shindano la Afya na Usala Kazini kutoka vituo na Mikoa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baadae ya kukabidhiwa Vikombe
Picha ya Pamoja Baina ya wafanyekazi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO baada ya Hafla ya kukabidhiwa Vikombe Washindi wa Shindano la Afya na Usalama Kazini Hafla iliyofanyika katika Kituo cha Kuzalisha Umeme Cha Kihansi.
Mhandisi Fredy Kayega Meneja wa Kitengo chá Afya na Usalama Kazini TANESCO Akizungumza katika Hafla ha Kuwapongeza Washindi wa Mwaka 2018/2019 katika kusimamia masuala ya Afya na Usalama Kazini Hafla iliyosogezwa Mbele kutokana na Janga la CORONA.  (Picha na Denis Mlowe)


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini