Hayo yamesemwa na Afisa elimu sekondari wilaya ya Mkuranga, Benjamini Majoha wakati akizungumza katika mahafali ya 19 ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya Ujenzi iliyopo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Amesema kuwa elimu ya kidato cha nne ndio ufunguo mhimu kwani kidato cha nne ndio kinarusu mtoto kuendela na kidato cha tano na cha sita au kujiunga na vyuo vya elimu ya kati.
Hata hivyo amewashauri wazazi na walezi wa watoto wasiwakatishe masomo watoto wao kwani elimu ndio ufunguo wa maisha.
"Mnapo maliza masomo yenu hapa mtumie elimu yenu kupambana na maisha, mmejifunza stadi za maisha darasani na kwa vitendo mkiwa shuleni makazitumie hizo kupambana na changamoto mbalimbali za maisha, msijiunge na tabia ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yenu hasa kupata mgonjwa mbalimbali pia msijiingize katika matumizi ya dawa za kulevya." Amesema Majoha.
Akijibu risala ya wanafunzi wanaohitimu amesema kuwa uhaba wa vitabu vya Kiada mesema kuwa teyari wameshaanza kushughulikia na hivi karibuni vitakuwepo vitabu hvyo kwaa utosherevu.
Nae Mkurugenzi wa Shule ya Ujenzi, Thadei Mtembei amesema kuwa shule ya Sekondari Ujenzi na shule nyingine dada kama St. Methews, St. Marks, Victory na shule ya msingi na Sekondari ya St. Methews ni shule zinazofanya vizuri kitaaluma kwa kidato cha nne kwa wanafunzi wanaofaulu vizuri mitihani yao huwa tunawapa unafuu wa kusoma bure kwa kidato cha tano na sita.
Kwa upande wa Mkuu wa Chule ya Sekondari ya Ujenzi, Josia Philipo amesema kuwa huduma zinazotolewa shuleni hapo ni nzuri na zinapelekea wanafunzu kufaulu mitihani yao vizuri.
Mafanikio kitaaluma yamekuwa makubwa kwa miaka mitatu mfululizo kwa kidato cha nne na kidato cha pili.
"Kwa mwaka 2017 matokeo ya kidato cha nne walifaulu kwa asilimia 98.3 na kidato cha pili walifaulu kwa asilimia 100, kwa mwaka 2018 na 2019 kidato cha nne walifaulu kwa asilimia 100 na kidato cha pili walifaulu kwa asilimia 100 pia." Amesema Philipo.
Kabla ya mahafali hayo walianza na kutembelea maonesho ya masomo kwa vitendo ambayo ya wanafunzi katika Shule hiyo ya Sekondari ya Ujenzi.
Hata hivyo Philipo amesema kuwa madarasa, mabweni, Mktaba, Maabara zenye vifaa vya kutosha, maji saa 24 umeme saa 24, kumaliza mapema Mhtasari wa masomo ndio siri kubwa ya mafanikio kwa shule ya Sekondari ujenzi.
Kabla ya mahafali hayo viongozi mbalimbali wametembelea maonesho ya masomo kwa vitendo ambayo ya wanafunzi amesoma darasanikatika Shule hiyo ya Sekondari ya Ujenzi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments