Charles James, Michuzi TV
Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amesema kwenye uchaguzi huu hakuna mbadala wa Rais Dk John Magufuli hivyo kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kumpigia kura nyingi ifikapo Oktoba 28 mwaka huu zitakazoweka rekodi ya Nchi.
Mavunde ameyasema hayo wilayani Mpwapwa alipokua akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene na kuwataka wananchi wa jimbo hilo kuonesha shukrani zao kwa vitendo kwa kumpigia kura Magufuli kwa mambo makubwa aliyowafanyia.
" Oktoba 28 naombeni mjitokeze kwa wingi mkampigie Magufuli kura za kishindo hadi wapinzania wapate aibu ili wakati mwingine wakome kuchukua fomu za urais tena, tunajua ameshashinda lakini nataka mkapige kura za aibu wapinzani waaibike siku hiyo, na hii ni kwa sababu ametutendea makubwa sisi watanzania na hasa nyie wananchi wa Kibakwe, Mpwapwa.
" Magufuli amewatendea makubwa watu wa Kibakwe, anapitisha reli ya umeme hapa kwenu ambayo ikikamilika itakua na uwezo wa kuwatoa hapa kuwapeleka Dar ea Salaam kwa masaa matatu tu mkauze mazao yenu na kurejea Dodoma hata mkiwa na mgonjwa Muhimbili unaweza kupika uji hapa na kumpelekea kila siku ni Magufuli peke yake anayaweza haya, mpeni kura Magufuli kwa miaka mitano tena akamilishe mengine makubwa," Mavunde.
Amewataka wananchi wao pia kumpigia kura mgombea ubunge wa jimbo hilo, George Simbachawene ili aweze kuchochea maendeleo kwa haraka kwani tayari anazijua njia za kuleta maendeleo na ni mtu ambaye uwezo wake ni mkubwa kiasi cha kuaminiwa na Rais Magufuli katika baraza lake la mawaziri.
" Dodoma tuna bahati ya Simbachawene kuteuliwa kwenye baraza la mawaziri hii ni wizara nyeti ambayo hadi Rais akuamini lazima uwe na uwezo, msimchukulie poa Simbachawene ameaminika na Nchi na nyie naombeni mumuamini," Amesema Mavunde.

Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma, Anthony Mavunde Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Kibakwe ambapo alienda kushiriki kumuombea kura Dk John Magufuli kwa ajili ya urais na George Simbachawene kwa ajili ya Ubunge pamoja na madiwani wanaotokana na CCM.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa, George Simbachawene akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni zake.
Viongozi na wananchi wa Jimbo la Kibakwe wakicheza muziki pamoja katika uzinduzi wa kampeni za Ubunge Jimbo hilo.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni Jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa, Dodoma wakifuatilia hotuba za viongozi kwenye mkutano huo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments