Askari Wamnusuru Bocco na Kipigo | ZamotoHabari.

 


KATIKA hali ya kushangaza mshambuliaji wa Simba, John Bocco, juzi alinusurika kupigwa na mawe na mashabiki wa timu hiyo kufuatia kitendo cha kukosa penalti katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao walichapwa bao 1-0.

 

Bocco alikosa penalti dakika ya 78 kwa shuti lake kugonga mwamba hali ambayo iliwakasirisha mashabiki kwa kuwa mchezo uliopita walifungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Championi ambalo lilikuwepo uwanjani liliwashuhudia mashabiki wakiwa wamejazana upande wa kutokea uwanjani huku wakidai wanamtaka Bocco na wengine wakiwa wameshika mawe mkononi.

 

Kitendo cha mashabiki hao kilipelekea Polisi kulazimisha basi la timu hiyo kuingia ndani ya uwanja kwa lengo la kuwatoa wachezaji huku ulinzi ukiwa umeimarishwa lakini haikuweza kuwafanya mashabiki hao kutoka katika eneo.

 

Hata hivyo basi la timu hiyo liliwachenga na kupitia kwenye geti lingine linalotazama na Uwanja wa Mkapa na kuondoka uwanjani hapo.


Stori: Ibrahim Mussa,Dar es Salaam



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini