Na Shukrani kawogo, Njombe.
Wakazi wa vijiji vya Luana, Mawengi na Mlangali wamemuomba Mbunge wa jimbo la Ludewa ambaye amepita bila kupingwa Joseph Kamonga kuwasaidia kumalizia ujenzi wa vituo vya afya ambavyo vimejengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara.
Ombi hilo wamelitoa wakati mbunge huyo alipofanya mikutano ya hadhata na wananchi wa vijiji mbalimbali vilivyomo katika kata hizo kwa lengo la kumuombea kura mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli.
Aidha kwa upande wa mbunge huyo alizipokea changamoto hizo na kuahidi kuzishughulikia Pindi atakapoapishwa na kuanza kazi rasmi.
“ Mkimchagua rais Dk. Magufuli mtakuwa mmenisaidia mimi kufanikisha maendeleo katika Jimbo letu kwakuwa mimi bila Dk. Magufuli ni sawa na bure kwani mipango yote tunayopanga hapa haitaweza kutimia kwakuwa yeye ndiye njia ya mafanikio”, Alisema Kamonga.
Alisema endapo Ludewa utampa rais Magufuli kura za kutosha itamsaidia kutembea kifua mbele na kuwa na nguvu ya kuwasilisha changamoto kwake.
Aidha kwa upande wa Diwani wa kata ya Luana ambaye naye amepita bila kupingwa pia ni Mkurugenzi wa taasisi ya PADECO Willbard Mwinuka ameahidi kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo ambapo ameahidi kuleta miradi ya maji katika vijiji vya Mlangali ndani na Ligumbilo.
"Endapo mtampa Dk. Mahufuli kura za kutosha na kumpitisha Diwani wa Chama Cha Mapinduzi naahidi kupitia taasisi yangu ya PADECO niko tayari kumsaidia diwani mwenzangu wa Mlangali Hamis Kayombo kwa kuleta mradi wa maji ili kuondoa kero mnayoipata". Alisema Mwinuka.
Mbunge huyo tayari ametembelea vijiji vijiji 18 ambapo vijiji 12 vipo katika tarafa ya Masasi na vijiji 6 vipo katika kata ya Mawengi ambapo zoezi hilo la kutafuta kura za Dk. Mahufuli litaendelea mpaka tarehe 27 mwezi huu na kila siku Mbunge huyo atafanya mikutano mitatu katika vijiji na kata mbalimbali.
Mbunge wa Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa wanakikundi Cha ufugaji kuku kilichopo kijiji cha Lugumbiro
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga aliyepita bila kupingwa akiwa na kundi la wananchi ambao walimuomba kumsindikiza kwa mguu kwa hatua kadhaa huku gari yake ilimfuata nyuma iliwa ni ishara ya upendo.
Katibu wa UWT wilaya ya Ludewa Flora Kapalia akiomba kura za Rais katikati Kijiji Cha Ikulu kilichopo kata ya Mawengi
Mbunge aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lupande kilichopo kata ya Mawengi
Diwani wa kata ya Luana Willba aliyepita bila kupingwa Wilg(Aliyevaa kofia, akiewa kwenye mkutano wa katikati Kijiji Cha Ikulu
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa ameshikana mkomo na mzee ambaye alimuimbia wimbo ambao alimtungia
Wajumbe wa kamati ya kampeni wilaya wakifuatilia mkutano uliokuwa ukiendelea katika Kijiji Cha mlangali ndani katika kata ya Mlangali
Kituo Cha afya Cha kinachojengwa katika Kijiji Cha Lupande kilichopo kata ya Mawengi

Mbunge aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akiwasaidia kupiga ngoma wanakikundi Cha ngoma alipowasili Kijiji Cha Lupande
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga aliyepita bila kupingwa (wameanza kushoto) akiwa na madiwani wakimuombea kura Dk. John Mafuli pamoja na Diwani wa kata ya Mlangali. Anayefuata ni Diwani wa kata ya Mawengi ambaye naye amepita bila kupingwa Leodgar Mpambalioto, na Mgombea udiwani wa kata ya Mlangali Hamis Kayombo.
Mbunge aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akisindikizwa na wananchi baada ya kumaliza mkutano
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments