LOWASA,KINANA WAMUOMBEA KURA DK.JOHN MAGUFULI ,WATOA SABABU | ZamotoHabari.


Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Arusha

WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa pamoja na Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Abdulrahman Kinana wamemuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya Chama hicho Dk.John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Arusha Mjini.

Wakizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Jiji la Arusha  wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais Dk.Magufuli ambaye leo amewaomba kura wananchi wa Mkoa wa Arusha ili achaguliwe tena kuongoza nchi kwa miaka mingine mitano.

Kinana na Lowassa walipata nafasi ya kuzungumza na kumuombea kura baada ya Dk.Magufuli kuwaomba viongozi hao wastaafu kuwasalimia wananchi waliokuwepo katika mkutano huo.

Kinana alikuwa wa kwanza kuzungumza na kisha kumuombea kura Dk.Magufuli ambapo anesema anaunga na Wana CCM wengine kumuombea kura mgombea huyo ambaye kwa kipindi cha miaka mitano amefanya mambo makubwa ya maendeleo.

Amefafanua Dk.Magufuli ameweza kutekeleza ahadi zote ambazo ziliahidiwa na CCM katika uchaguzi mkuu mwaka 2015, ametekeleza ahadi zote alizoahidi akiwa katika ziara zake za mikoani, na sasa anatoa ahadi nyingine kupitia Ilani ya CCM yenye kurasa 303,hivyo kuna kila sababu ya kumchagua Oktoba 28 mwaka huu.

Kwa upande wake Lowassa hivi sasa kuna nchi kadhaa ikiwemo ya Venazuela na Nigeria kuna vurugu kwa mambo ambayo yanaleta amani nchini Tanzania."Kupitia kwa Mwenyezi Mungu,Rais wetu amepewa jukumu la kuangalia mambo katika nchi hii amekuja na ndoto sahihi kwamba madhara hayo hayaji kwetu...amejitahidi na wananchi wameelewa,"amefafanua Lowassa.

Amesema kwa mambo makubwa ambayo yamefanywa na Rais,zawadi pekee ambayo wananchi wanatakiwa kumpa ni kumpigia kura Oktoba 28 ambayo ndio siku ya Uchaguzi Mkuu nchini.




APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini