OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA YAWAHAKIKISHIA WANANCHI SONGWE KUTENDA HAKI NA KUWAONDOLEA MALALAMIKO YAO YA MUDA MREFU. | ZamotoHabari.


 
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga


Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imewahakikishia wananchi wa Mkoani Songwe kutenda haki na kuwaondolea malalamiko ambayo yalikuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa ukaribu wa huduma za kiofisi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga ameeleza "Yeyote atakayefanya fujo kipindi hiki ama kipindi chochote kile waache mara moja, kwani serikali haiwezi kuwavumilia hao wote waliopanga kufanya fujo".

Aidha Katika hatua nyingine Bw. Mganga ameongeza kuwa tayari watu 24 Tunduma Mkoani Songwe wametiwa mbaroni kutokana na kujihusisha na vurugu zilizosababisha mauaji ya kijana mmoja mpakani hapo.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Songwe.

Mkurugenzi wa Mashtaka aliendelea kueleza kuwa amewahakikishia upatikanaje wa haki baina ya wananchi Mkoani Songwe huku akisisitiza kuwa kutokana na Mkoa huo upo mpakani hivyo atahakikisha wanafungua Ofisi nyingine mpakani Tunduma kwa lengo la kuzuia uhalifu wa kimpaka.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangala alimpongeza Mkurugenzi wa Mashtaka pamoja Ofisi yake kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhakikisha haki, amani vinapatikana katika nchi hii.

Akiendelea kueleza kuwa licha ya Mkoa wa Songwe kuwa ni mchanga lakini uhitaji wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ulikuwa ni mkubwa kutokana na Mkoa huo kuwa upo mpakani na una mwingiliano mkubwa wa watu, hivyobasi uwepo wa Ofisi hiyo kuwa karibu utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kupunguza malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wananchi juu ya ucheleweshaji wa upatikanaji wa haki.

Naye pia Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Songwe Bw. Kassim Mkwawa ameeleza kuwa uwepo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Songwe utarahasisha majadala ya kesi mbalimbali za uchunguzi kushughulikiwa kwa haraka, ambapo awali yalikuwa yakipelekwa Mbeya na kutumia muda mrefu kufanyiwa kazi.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo pia ametoa shukrani kwa viongozi wa dini kwa namna wanavyoliombea Taifa pia amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Songwe juu ya Mtumishi yeyote wa Serikali atakaebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa Ofisi yake haitosita kusaini barua ya kumsimamisha kazi, Kwan kufanya hivyo ni kukandamiza haki za watu wengine.

Baadhi ya wadau Mkoani Songwe wamesema uwepo wa Ofisi hiyo ni kupunguza umbali wa kupata huduma na kuondoa malalamiko baina ya wananchi.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini