Mimba za Mobeto kwa Mondi Zamshtua Zari | ZamotoHabari.



KAULI ya mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto aliyoitoa hivi karibuni kuwa, alinasa mimba tatu za mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi zikaharibika, ni kama zimechoma kichaka, Risasi Jumamosi limenasa ishu.


 


Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye ni raia wa Uganda na mama wawili wa Mondi, ambaye ni msanii nguli Bongo, ameibuka na kushtushwa na kauli hiyo na kusema:


 


“Kiko wapi, kila kitu kimejifunua wazi, niliposema waliniona muongo,” Zari alinukuliwa na mtandao mmoja wa kijamii nchini Uganda unaodai kuzungumza naye kuhusu kauli ya Mobeto kumhusu mzazi mwenzake.


Zari aliyezaa watoto wawili na Mondi, alivunja uhusiano na kutimkia Afrika Kusini kutokana na kile alichodai kuwa, Diamond hakuwa mwaminifu.


 


Inadaiwa kuwa, wakati Zari akiishi Madale, jijini Dar es Salaam na Mondi kama mke, mzee baba alikuwa akichachua mahaba na Mobeto kwa siri.


Hatima ya mapenzi ya siri ya Mondi na Mobeto, ni kupatikana kwa mtoto mmoja wa kiume, ambapo Mobeto anasema siyo huyo tu, bali kuna mimba nyingine tatu ziliharibika.


 


Maoni katika mtandao wa kijamii nchini Uganda ulioandika habari ya Zari kushtushwa na kauli hiyo ya Mobeto yaliyotupiwa na baadhi ya watu kwa lugha ya Kiingereza na Risasi kuyatafsiri, yalisomeka:


“Bora ulivyojiondokea zako, huyo mwanaume hakuwa anatosheka na wewe.”


“Amefichua siri ya usaliti wao, mwanamke hana haya huyu.”


“Acha maisha yaendelee Zari.”


 


Hata hivyo, mtandao huo haukuweka bayana mshtuko wa Zari unatokana na nini, kwani kama penzi la Mondi tayari ameshalitema na yeye amebakia kuwa mama wa watoto wa msanii huyo.


Mara kadhaa Zari amekuwa akizipuuza taarifa za ma-eksi wa Mondi kwa kusema, hana cha kupoteza kwani maisha yanaendelea.


 


Akizungumza na chombo kimoja cha habari wiki hii, Mobeto alijimwambafai kuwa:


“Kwanza kabisa, nadhani katika mtu ambaye alikuwa na uhakika wa Dylan kuwa ni mtoto wake, nadhani Diamond alikuwa wa kwanza, kwa sababu kabla sijamzaa Dylan, niliwahi kupata mimba tatu.


 


“Ujauzito wa kwanza ulitoka, sijui tulienda nchi gani mimba ikatoka kwa bahati mbaya, nikaja nikapata ya pili ikatoka, mpaka ya tatu nayo ikatoka na kipindi chote hicho tupo pamoja.


 


“Kwa hiyo, huyu Dylan ilikuwa mimba ya nne na kipindi chote cha ujauzito, tulikuwa pamoja mpaka siku naenda kujifungua, lakini siyo kwamba nilimtegeshea Diamond mimba kama ambavyo watu wanazungumza.


 


“Ila kutokana na maneno ya watu kuwa mengi, kuna siku Diamond alinitumia meseji akaniambia Hamisa maneno kwa upande wangu yamekuwa mengi sana, najua kwamba siyo sawa ila naomba tukafanye DNA (kupima vinasaba) kwa ajili ya mtoto, nikamwambia sawa.


 


“Siku ya Jumatano au Jumanne hivi akanipigia tena akaniambia amepata appointment na daktari, hivyo nijiandae kwa ajili ya kwenda kupima, kweli mwisho wa siku tukaenda kupima.


“Baada ya hapo tukaambiwa tusubiri majibu baada ya wiki tatu au nne, majibu yakatoka kwa asilimia zote kuwa Dylan ni mtoto wake.”



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini