TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imekutana na watazamaji wa uchaguzi kutoka nje na ndani ya Tanzania kuelezea matayarisho ambayo imefanya na yale ambayo inaendelea kuyafanya na kwa kiasi kile ambacho Tume imejiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo.
NEC imekutana na watazamaji hao ambapo pamoja na mambo mengine watazamaji hao wameelezea kufurahishwa na maandalizi yanayoendelea kufanywa kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Watazamaji hao wamezungumzia pia mchakato huo wa NEC ambavyo umekuwa wa uwazi kwa watu wote ambao umeendelea mpaka sasa na suala kubwa lilikuwa ni kuendelea kuwahimiza watu kuzingatia sheria, wazingatie taratibu ili siku hiyo ya uchaguzi watakapoenda kupiga kura kwa wamani.
Akizngumza mbele ya watazamaji hao, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria NEC Emmanuel Kawishe amefafanua kwamba watazamaji wenyewe wamesisitizana kufuata sheria , kuzingatia miongozo iliyotolewa na Tume ili uchaguzi uendelee kuwa wa amani maana kuna maisha baada ya uchaguzi.
"Wawakilishi wa taasisi zote za kimataifa ambazo ziko 17 na tunawawakilishi kutoka taasisi za ndani ambazo ni 97, tumekuwa na wawakilishi kutoka kila taasisi na kila moja imeleta wawakilishi zaidi ya wawakilishi wanne.Pia tulikuwa na Rais mstaafu wa taifa la Burundi ambaye naye alikuwa katika misheni yetu tuliyokuwa nayo hapa,"amesema Kawishe.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema unapokuwa mtazamaji haina maana unaweza kuwa juu ya sheria na kwamba unaweza kutoka nje lakini usipofuata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na usipofuata sheria ambazo zipo hapa nchini unaweza kujikuta unakuwa muhalifu na sheria itachukua mkondo wake.
"Kwa hiyo nilikuwa nasisitiza suala hilo kwamba pamoja na kuwa waangalizi hao ni wageni kwa ajili ya kutazama uchaguzi ambao tunatarajia kuufanya lakini ni vema wakajitahidi kutovunja sheria kwani wakizivunja sheria itachukua mkondo wake.
"Lakini nawakumbusha hawa waangalizi au watazamaji wa hapa nchini kwamba tumeshapewa hii nafasi basi serikali imeona unafaa kuwa mtazamaji , basi kikubwa ni kwamba usivunje sheria ,na jaribu sana kuhakikisha wanatenda haki ,wanashauri jambo ambalo ni la haki wasiingie tena katika mambo ya ushabiki , kwani wakishaingia katika ushabiki mwisho wa siku unajikuta umeingia kwenye uhalifu na tutashughulika kama tunavyoshughulikia wahalifu wengine,"amesema IGP Sirro.
Amesisitiza cha msingi mazungumzo yalikuwa mazuri kati yao wadau na NEC , kwani wamekumbushwa kuzingatia wajibu wao , jeshi limekumbusha wajibu wao na watazamaji nao wamekumbushwa kutimiza wajibu wao , hivyo amepata faraja kuona kila mdau ametakiwa kutimiza wajibu wake.
Kamishina wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Balozi Omari Ramadhani Mapuri akizungumza mbele ya Watazamaji wa Uchaguzi Mkuu 2020 wa Ndani na NJe ya Tanzania jijini Dar walipokuwa wakielezwa matayarisho ambayo imefanya na yale ambayo inaendelea kuyafanya na kwa kiasi kile ambacho Tume imejiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020 nchini kote.Picha na Michuzi JR-MMG.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza mbeleya viongozi Waandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Watazamaji wa Uchaguzi Mkuu 2020 wa Ndani na NJe ya Tanzania,namna Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuhakikisha Uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu.
Sehemu ya meza kuu ya Viongozi Waandamizi wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), wakifuatilia yaliyokuwa yakielezwa ukumbini humo.
Baadhi ya Watazamaji wa uchaguzi kutoka nje na ndani ya Tanzania wakifuatilia yaliyokuwa yakielezwa na Tume ya Uchaguzi kuhusu namna ilivyojiandaa kuhakikisha uchaguzi unakuwa Huru na wa Haki na kwa utulivu mkubwa.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Simon Sirro akifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa na Tume ya Uchaguzi katika kikao hicho muhimu cha kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unafanyika kwa utulivu mkubwa.
Watazamaji kutoka Nje ya Nchi wakifuatilia kwa makini maelezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi,namna ilivyojiandaa kufanikisha shughuli nzima ya Uchaguzi Mkuu 2020,unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020 nchini.
Baadhhi ya Watazamani wa ndani wa Uchaguzi wakichangia mawazo yao katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa Amani na utulivu nchini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Simon Sirro akifafanua jambo kwenye kikao hicho kilichowakutanisha watazamaji wa uchaguzi kutoka nje na ndani ya Tanzania ,ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa ikieleza matayarisho ambayo imefanya na yale ambayo inaendelea kuyafanya na kwa kiasi kile ambacho Tume imejiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments