SERIKALI YATOA FEDHA KUKAMILISHA UJENZI JENGO LA OFISI YA TAKWIMU MKOA WA KIGOMA | ZamotoHabari.


Na Editha Karlo,Kigoma.


SERIKALI  imetoa  zaidi ya Shilingi milioni 600 kwa ajili kukamilisha ujenzi wa jengo la  Ofisi ya Takwimu Mkoa wa kigoma baada ya kukaa kwa zaidi ya miaka 26 bila kukamilika tangu kuanza kujengwa.

 Afisa Mkuu wa Takwimu wa Serikali Albina Chuwa ameyasema hayo  wakati wa hafla ya kutiliana saini mkaba wa kujenga ofisi ya Takwimu ya Mkoa wa Kigoma (NBS) na Wakala wa majengo TBA Mkoa wa Kigoma.

Ambapo wakala hao majengo  wamepewa miezi miwili tu kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ambalo limeanza kujengwa tangu mwaka 1994.

"Serikali yetu tayari imeshatoa milioni 600 kwaajili ya ujenzi wa ofisi hii,Ujenzi huu unatakiwa ukamilike ndani ya miezi miwili kwani jengo hili limeanza kujengwa muda mrefu toka mwaka 1994 hadi leo"alisema

Naye Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Kigoma Julias Daniel, amesema watahakikisha wanafanya uboreshaji wa ofisi hiyo kwani tayari wameshapata michoro ya ramani itakayorahisisha kukamilisha kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa Kigoma Thobias Andengenye, amewataka kuanza mara moja ujenzi wa jengo hilo ili kurahisha kuweka takwimu za mkoa vizuri kwani ni muhimu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.

Amesema ukosefu wa takwimu ni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kurudisha nyuma maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Jengo la ofisi ya takwimu lilianza kujengwa mwaka 1994 lakini mpaka sasa halijakamili licha ya kupigiwa kelele kila mwaka na mamlaka husika.

Mkurugenzi mkuu wa Takwimu wa serikali Tanzania(NBS)Dkt Albina Chuwa (kushoto)na Meneja wa Majengo wa Mkoa wa Kigoma Julias Chego wakipongezana baada ya kutiliana sahini ya mkataba wa ujenzi wa ofisi ya Takwimu Mkoa wa Kigoma anaye shuhudia katika ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye.
Mkurugenzi mkuu wa Takwimu wa serikali(NBS)Dkt Albina Chuwa(kushoto)na Julias Chego meneja wakala wa majengo(TBA)wakionyesha mikataba waliyosaini ya kujenga ofisi ya Takwimu ya Mkoa wa Kigoma,katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini