STAA wa muziki wa Afro – R&B nchini Nigeria, Simisola Kosoko a.k.a Simi amefunguka kuwa, anatamani kuwaona mastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zuhura Othman ‘Zuchu’ wakifunga ndoa. Diamond na Zuchu ni wasanii walio chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) huku Mondi akiwa ndiye mmiliki wake.
Ingawa Zuchu bado ni msanii mchanga lakini moto wake anaouonyesha kwenye game ndiyo uliofanya aingie kwenye levo za ustaa fasta.
Akipiga stori na gazeti hili kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii kutoka Nigeria, Simi amemwambia mwandishi wetu kuwa, anavutiwa sana na Mondi na Zuchu kiasi cha kutamani kusikia ndoa yao ikifungwa hata kesho. “Nawapenda sana hao wasanii, siwezi kufi cha hisia zangu. Wanapendezea sana,” anasema Simi na kuongeza: “Unajua muziki unakua, unasafi ri na kufi ka mbali.
Kwa sisi wasanii wa Afrika, tunajisikia fahari kutanua mashabiki wetu hasa ndani ya bara letu kabla ya kutusua zaidi nje. “Sababu hiyo imenifanya niwe mfuatiliaji sana wa wasanii wa ndani ya Afrika… na katika hili lazima niwe mkweli, wasanii wa Afrika Mashariki wanafanya kazi nzuri sana.
Kwa mfano Uganda, nawafuatilia sana wasanii kama Navio (Daniel Lubwama Kigozi) na zamani kidogo Jose Chameleon.
“Kenya nilikuwa nikizimika sana na Nazizi, lakini kwa wasanii wa sasa nawapenda zaidi Sauti Sol. Kwa hapo Tanzania, msanii wangu wa muda wote ni Diamond. Huyo bwana anajua sana.”
Anasema kwa sababu ya kuvutika na muziki wa Bongo Fleva na hasa msanii Diamond kama chaguo lake, amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana.
“Nasoma sana mitandao, ni kweli sijui Kiswahili kabisa, lakini mitandao mingi ya Kenya na Uganda hutumia Kiingereza, lugha ambayo naifahamu, inanisaidia kujua kinachoendelea kwenye muziki wa Afi ka Mashariki.
“Kwa sasa naona habari za moto zinasema Diamond na Zuchu ni wapenzi, kama ni kweli ni kitu kuzuri na kiukweli natamani sana wafunge ndoa.
Wanapendezeana sana,” Simi anazidi kumwaga baraka zake kwa wasanii hao. Simi ambaye mwezi huu amedondosha singo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘No Longer Benefi cial’ ni mke wa msanii wa muziki na mbunifu nchini humo, anayekwenda kwa jina la Adekunle Gold.
Anasema, anajisikia huru kuoana na msanii huyo kwa sababu wanafahamiana vizuri na anampa mwongozo na sapoti kubwa kwenye muziki. Simi ameshatoa nyimbo kadhaa akishirikiana na mumewe, Gold, ukiwemo ‘No Forget’ unaofanya vizuri kwenye game.
Akizidi kushusha mistari kwa wasanii hao, Simi anasema: “Kuna raha fulani hivi ya kipekee unaipata kwa kuoana na mtu ambaye mnayefanana vitu mnavyofanya. Najua ninachosema maana nipo kwenye ndoa na mtu wa aina hiyo.
“Diamond na Zuchu wakifanya hivyo, wataipata raha hiyo, lakini pia watakuwa huru zaidi kufanya kazi kwa ufanisi, ukaribu na mafanikio zaidi.”
Simi anasema kwa uzoefu wake, ndoa nyingi za mastaa wanaooana na wasio maarufu huvunjika mapema, huku akitaja sababu kubwa kuwa ni kutokuendana. “Lakini mkioana wasanii mnakuwa mnazungumza lugha moja, ndiyo maana nitajisikia raha sana siku nikisikia Zuchu na Diamond wamefi kia hatua hiyo,” anasema.
UHUSIANO WA ZUCHU NA DIAMOND
Nyota ya Zuchu imeanza kung’ara akiwa na WCB chini ya Diamond na tangu amechomoka moto wake haujawahi kuzima. Hata hivyo kumekuwa na tetesi za muda mrefu kwamba wawili hao wamekuwa wakitoka.
Uhusiano wao umekuwa ukishabikiwa na wengi, lakini hakuna yeyote kati yao aliyejitokeza kuthibitisha au kukanusha kuhusu uwepo wa uhusiano huo. Mashabiki wengi waliotoa maoni yao mitandaoni kuhusu uhusiano wao, wameonekana kuunga mkono kapo hiyo.
DIAMOND NA UHUSIANO
Historia ya kimahusiano ya Diamond in aonyesha namna anavyopenda kutoka na mastaa. Baadhi ya mastaa aliowahi kutoka na kudumu kwa muda mrefu kabla ya kuachana ni pamoja na Wema Sepetu (mwigizaji – Bongo), Penniel Mungilwa ‘Penny’ (Mtangazaji – Bongo) na Jacqueline Wolper (Mwigizaji – Bongo).
Mbali na mastaa hao, amepata kutoka na mjasiriamali wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili.
Aidha, amekuwa kwenye uhusiano na mwanamuziki na mwanamitindo wa Kibongo, Hamisa Mobeto ambapo walibarikiwa kupata mtoto mmoja.
SIMI NI NANI?
Anaitwa Simisola Kosoko, lakini mwenyewe alifupisha jina lake na kuwa Simi. Alizaliwa mwaka 1988, Yaba / Ojuelegba, jijini Lagos – Nigeria. Kipaji chake kilianza kuchomoza tangu akiwa mdogo, ambapo alikuwa akiimba na kucheza kwenye kwaya ya kanisani kwao huko Lagos, Nigeria.
Baadaye alipokuwa mkubwa, aliingia rasmi kwenye muziki mwaka 2014. Baadhi ya nyimbo zake zilizofanya vizuri tangu wakati huo ni pamoja na ‘Tiff’, ‘Jamb Question’ na ‘Love Don’t Care’ alizoimba peke yake.
Nyimbo alizoshirikiana na wasanii wengine ni pamoja na Solder (Falz), No Forget (Adekunle Gold – mumewe) na ‘So Rire’ (Legendury Beatz). Alifunga ndoa na Gold, Aprili mwaka jana.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments