Kocha Sven Atoa Sababu za Kiwango cha Simba Hivi Sasa Kushuka | ZamotoHabari.



Kocha Mkuu wa Kikosi cha Simba Mbeligiji Sven Vanderbroeck amesema wachezaji wake wanaandamwa na uchovu mkubwa kufuatia michezo mfululizo wanayocheza na kukosa muda wakutosha wa kupata mapumziko ya wachezaji hayo.



Sven ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo wa Simba dhidi ya Simba kumalizika saa tatu usiku wa hapo jana kwa Simba kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye dimba la mkapa jijini Dar es Salaam.


“Tumetoka Mbeya tumepata mapumziko ya siku mbili na sio nne ili kucheza na KMC, na baada ya mchezo wachezaji 5 hadi 6 walikuwa wanajilaza wamechoka sana lakini wamecheza na kupata ushindi inamaanisha wachezaji wamejitoa kwa kila kitu”.


Kuzungu ubora wa wapinzani wake KMC aliocheza nao usiku wa hapo jana Sven amesema “Kabla ya mchezo niliwaambia utakuwa ni mchezo wa kimbinu sana, KMC ni moja ya timu bora sana kwenye ligi na wazuri kwenye nafasi. Dk90' zimeonesha tumejitoa kwa kila kitu kushinda”.


“Wakati mwingine ushindi kwenye michezo migumu inakufanya uwe bingwa, Hii michezo mibaya yenye upinzani wa asilimia hamsini ya kushinda kwa kila mmoja ukiishinda inakufanya uende mbali, uwe bingwa”.


Baada ya mchezo huo, Simba inataraji kusafiri siku ya kesho kuelekea Zimbabwe na msafara wa wachezaji 22 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa hatua ya mtoano ya pili kuwania kufuzu kutinga makundi michuano ya klabu bingwa barani Africa.

 



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini