Rekodi mpya ya Kagere mbele ya wachezaji wengine | ZamotoHabari.

 


Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda na klabu ya Simba SC, Meddie Kagere amefikisha mabao 50 ya ligi kuu Tanzania bara hapo jana kwenye mchezo dhidi ya KMC huu ukiwa ni msimu wake wa 3, takwimu zinaonyesha Kagere ndio mchezaji aliyefikisha mabao 50 ya VPL haraka zaidi kuliko mchezaji yoyote


Usiku wa jana katika mchezo wa ligi kuu kati ya Simba SC  na KMC ambao ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penati dakika ya 77, bao, hilo la Kagere linakuwa bao lake la 5 msimu huu wa 2020-21 ambao bado unaendelea. 


Mshambuliaji huyo alijiunga na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, kwa misimu 3 mfululizo akitokea Gor Mahia FC ya Kenya msimu wa 2018-19.


Kwenye msimu wake wa kwanza wa 2018-19 Kagere alifunga mabao 23, msimu uliofuata wa 2029-20, alifunga mabao 22 na misimu yote hii miwili alimaliza akiwa kinara wa ufungaji. Ukichukua idadi ya mabao aliyofunga misimu miwili iliyopita na ukajumlisha na mabao 5 ya msimu huu anakuwa amefunga jumla ya mabao 50 ya ligi kuu ndani ya misimu 3 ingawa msimu huu wa 2020-21 bado unaendelea.




Inaaminika Meddie Kagere ndio mchezaji aliyefikisha mabao 50 ya ligi kuu soka Tanzania bara haraka zaidi kuliko mchezaji yoyote yule, kutokana kutokuwa na utunzanji mzuri wa takwimu za ufungaji, ila bado ukirejea kwa wadau mbalimbali na wafuatiliaji wa soka hapa nchini wanaamini hakuna mchezaji aliyewahi kuwa na wastani mkubwa wa ufungaji kwa misimu 3 mfululizo kama Kagere.


Rekodi nyingine kubwa ya ligi kuu ambayo inaangaziwa kama kagere anaweza kuifikia au kuivuka ni ile iliyowekwa na Mohamed Hussein maarufu Mmachinga mwaka 1999 takribani miaka 21 iliyopita, ya kufunga mabao 26 ya ligi ndani ya msimu mmoja wa ligi kuu.

 



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini