Wanajeshi wa serikali wamezingira eneo ambalo watu waliojihami kwa bunduki wanaaminiwa kuwashikilia mateka watoto wa shule katika eneo la kaskazini - magharibi mwa Nigeria, msemaji wa Rais Muhammadu Buhari amesema.
Watoto 10 wameripotiwa kushikiliwa mateka, Garba Shehu amesema, idadi ambayo ni ndogo kuliko ile iliyoripotiwa na wafanyakazi kutoweka.
Karibi wanafunzi 800 wanasoma katika shule hiyo ya bweni ya wavulana katika jimbo la Katsina na karibu nusu yao hawajulikani waliko.
Washambuliaji wanasadikiwa kutaka kulipwa kikombozi, Bwana Shehu amesema.
Serikali imetaja washambuliaji hao kuwa majambazi, jina linalotumika kuashiria genge linalohudumu katika eneo hilo.
Shirika la kutetea haki la Amnesty International linasema watu 1,100 waliuawa na majambazi kaskazini mwa Nigeria katika mizi sita ya kwanza ya mwaka huu, lakini serikali imeshindwa kuwachukulia hatua washambuliaji hao.
Mwandishi wa BBC Nigeria Mayeni Jones amesema kumekua na ongezeko la wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Nigeria.
Eneo la kaskazini - magharibi limeathiriwa zaidi na utekaji wa kutafuta kikombozi, eneo la kaskazini mashariki linahangaishwa na wanamgambo wa Kislamu, huku eneo la kusini likikabiliwa na mashambulio kutoka kwa makundi yanayolenga viwanda vya mafuta vikitaka mgao wa mapato ya mafuta, aliongeza kusema.
Wazazi wamekusanyika katika shule hiyo iliyopo eneo la Kankara, wakitoa wito kwa mamlaka kuwasaidia kuwapata watoto wao, Shirika la habari la Reuters limeripoti.
Mzazi Abubakar Lawal alinukuliwa kusema kwamba watoto wake watatu waliokuwa wakisoma katika shule hiyo hawajulikani waliko.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments