Tanzia: Waziri Ng’wandu Afariki Dunia | ZamotoHabari.


MBUNGE wa zamani wa Maswa na waziri mstaafu, Dkt. Pius Yasebasi Ng’wandu, amefariki dunia katika Hospitali ya Somanda, Bariadi mkoani Simiyu alipokuwa akipatiwa matibabu kwa matatizo ya presha.

Ng’wandu aliwahi kuwa Mbunge wa Maswa, pia Waziri wa Ardhi, Maji, Nyumba na Maendeleo ya Mji kuanzia mwaka 1985 hadi 1987, na  alikuwa Waziri wa Maji 1987 hadi 1990, nafasi ambayo aliishika tena mwaka 1996 hadi 1999.

Hivi karibuni, alivuma mitandaoni baada ya kufunga ndoa na binti mwenye umri mdogo zaidi kuliko yeye ambapo baadhi ya watu walidai kuwa ana umri wa mjukuu wake



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini