TAWA YAZINDUA RASMI BUCHA YA KWANZA YA WANYAMAPORI NCHINI | ZamotoHabari.

 


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis R. Semfuko Leo tarehe 20/12/2020 Jijini Dodoma amezindua bucha ya kwanza ya nyamapori nchini kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa mapema mwaka huu.


Hafla hizo za Uzinduzi zilifanyika maeneo ya chang'ombe Mtaa wa Stendi ya Zamani Makao Makuu ya Nchi Dodoma, ambapo Mwenyekiti huyo wa Bodi aliambatana na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Bw. Mabula Misungwi pamoja na wajumbe wa Bodi hiyo ya TAWA.

Aidha, bucha hii imekuwa ya kwanza kati ya bucha 46 zilizopata usajili baada ya Kamati ya Kumshauri Kamishna kuhusu bucha za kuuza nyamapori kuridhia kufuatia kanuni ya  bucha ya mwaka 2020  ambayo iliundwa baada ya Tamko la Mh.Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli la Mwezi  Machi mwaka huu kutaka kuanzishwa bucha za nyamapori Tanzania.

Wananchi wa Viunga vya jiji la Dodoma leo walifurika maeneo ya chang'ombe kushuhudia zoezi hilo la Uzinduzi na kufurahia fursa ya kupata kitoweo adimu cha Nyamapori, ambapo Mara baada ya zoezi la Uzinduzi wananchi hao walijaa katika bucha hiyo inayomilikiwa na Mfanyabiashara aitwaye Bw.Samson Joel  Kitangengi na kujinunulia kitoweo hicho.

TAWA imetekeleza kikamilifu agizo la Rais wetu na hivyo ni imebaki zamu ya wananchi wa Tanzania kufurahia fursa hadhimu ya  rasilimali za wanyamapori wetu.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini