Anemia hali inayotokea pale kiasi cha seli nyekundu za damu zinapokuwa chache kuliko kawaida au seli hizi nyekundu zinapungukiwa na chembechembe za hemoglobin kwa lugha rahisi tunasema ni upungufu wa damu mwilini.
Kuishiwa damu hupelekea mwili kuwa mchovu muda mwingi, misuli kuishiwa nguvu, mood kubadilika na kupata ganzi mara kwa mara. Tatizo linavokuwa kubwa zaidi linaweza kupelekea matatizo kwenye moyo, ubongo na viungo vingine vya mwili.
Hivyo ili kuepukana na kupatwa na upungufu wa damu mwilini zifutazo ni hatua za kuongeza damu mwilini:
Kuimarisha ufanyaji kazi wa Bandama
Bandama ni kiungo kinachohusika na utengenezwaji wa seli nyekundu za damu na pia kuweka msawazo wa majimaji mwilini. kama bandama yako ina shida basi hii ni sababu ya kwanza kwanini una upungufu wa damu mwilini.
Tumia vyakula vifuatavyo ili kuweka sawa bandama yako.vyakula kama spinach na mboga zingine za kijani, maboga na mbegu za maboga na karanga.
kuimarisha mfumo wa chakula
Hatua ya kusafisha na kuimarisha mfumo wa chakula ni muhimu sana kutokana na kwamba unaweza kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi lakini mwili ukafeli kuvyonza madini kuingia kwenye damu. Tatizo ni kwamba una hali inayoitwa leaky gut syndrome.
Angalia mfano huu ili unielewe kuhusu leky gut syndrome. Utumbo mwembamba ndio huusika na uchakataji wa chakula na kisha virutubisho muhimu kuruusiwa kuingia kwenye damu na makapi zikiwemo sumu, virusi, bacteria na vimelea wabaya kutolewa nje. Sasa ukuta huu ni kama chekecheke linachuja vitu vizuri na vibaya.
Chekecheke hili linapotoboka kutokana na ulaji wa vyakula hatarishi na uwepo wa fangasi linaanza kuruhusu sumu na vitu hatari kuingia kwenye damu, kitendo hichi cha kutonoka kwa chekecheke kwenye utumbo na tumbo tunaita leaky gut na mkusanyiko wa dalili mbaya zinazotokana na sumu, vimelea na takataka kuingia kwenye damu kama alegi, kichefuchefu na mwili kutosaga chakula vizuri tunaita leaky gut syndrome.
Hatua ya tatu ni kutumia kwa wingi vyakula vyenye madini ya chuma
Hatua inayofuata katika kuimarisha utengenezwaji wa seli nyekundu za damu ni kuongeza kweye sahani yako vyakula vyenye madini chuma kwa wingi. Vyakula hivi ni kama Nyama, samaki, karanga, maharage na mboga za kijani kama spinach. viungo kama maini ya madini chuma kwa wingi zaidi.
Hatua ya nne ni Kupunguza msongo wa mawazo
Kama unapata msongo wa mawazo, hasira, hofu na kushindwa kusamehe watu basi unapunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa bandama yako. Hivo hakikisha unakuwa na ratiba ya kupumzika na kufurahia maisha, na kupata usingizi wa kutosha.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments