Serikali yakanusha hospitali kujaa wagonjwa wenye shida ya mfumo wa hewa | ZamotoHabari.





Katibu Mkuu Wizara ya Afya nchini Tanzania, Profesa Mabula Mchembe amesema hospitali hazijajaa wagonjwa wenye shida ya mfumo wa hewa kama inavyoelezwa, akibainisha wengi wapo katika wodi za upasuaji.


Profesa Mchembe ameyasema hayo leo Jumamosi  Februari 13, 2021 alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) pamoja na kuangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za afya katika hospitali hiyo.



"Wafanyakazi wanaohudumia wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa hewa wana afya njema wala hawajapata matatizo. Ukiangalia hospitali sio kama wanavyosema kwamba zimejaa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa hewa, hapa nimekuta wagonjwa wengi zaidi katika wodi za upasuaji," amesema Profesa Mchembe.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Amebainisha kuwa kwa sasa wataongeza nguvu katika upande wa upasuaji ili wananchi wasikae hospitali kwa muda mrefu.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini