Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa Maji safi na Salama na Mazingira katika Eneo la Usambazaji Maji Kisarawe, Pugu na Gongolamboto Mkoa wa Dar es salaam leo Febuari 13,2021. Makamu wa Rais yupo katika ziara ya siku mbili ya kikazi ya kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maji na Mazingira katika Mkoa wa Dar es salaam leo Febuari 13,2021. katikati ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu, kushoto ni Mtendaji Mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemenja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Nyumba aliyokuwa akiishi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati alipokuwa akifundisha Shule ya Pugu Sekondari kuanzia mwaka 1952 hadi mwaka 1955 iliopo Pugu Juu mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji safi na Salama, alipokuwa katika ziara ya kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maji na Mazingira Mkoa wa Dar es salaam leo Febuari 13,2021. . katikati ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu, kushoto ni Mtendaji Mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemenja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu Juu baada ya kuzindua Mradi wa Maji safi na Salama katika Eneo hilo leo Febuari 13,2021. Makamu wa Rais Yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maji na Mazingira Mkoa wa Dar es salaam leo Febuari 13,2021.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments