RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA SALA YA IJUMAA NA KUMUOMBEA DUA MAREHEMU SAYYID HUSSEIN BADAWY | ZamotoHabari.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi wa Dini baada ya kumalizika kwa Dua ya kumuombea Mwachuoni Mkubwa Afrika Mashariki Sayyid Hussein Badawy, iliofanyika katika Masjid Mushawr Muembeshauri Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) 

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza na kutowa wasifu wa Mwanachuoni Mkubwa Afrika Mashariki na Kati Marehemu Sayyid Hussein Badawy, wakati wa kumuombea dua iliofanyika Masjid Mushawr Muembeshauri Jijini Zanzibar na (kulia) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ungyuja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana.(Picha Ikulu)

KATIBU wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume akiwasailisha salamu za Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wakati wa hafla ya kumuombea dua Mwachuoni Mkubwa Afrika Mashariki na Kati Marehem Sayyid Hussein Badawy, iliofanyika katika Masjid Mushawr Muembeshauri Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiitikia dua ya kumuombea Marehemu Sayyid Hussein Badawy baada ya kumalizika Sala ya kumuombea iliofanyika katika Masjid Mushawr Muembeshauri Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiitikia dua ikisomwa na Naibu Mufti Mkuu Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa, kumuombea Marehemu Mwanachuoni Mkubwa Afrika Mashariki na Kati Sheikh Sayyid Hessein Badawy, iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Jijini Zanzibar, na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe. Rashid Simai Msaraka na (kushoto kwa Rais) Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar katika Sala na Dua ya kumuombea Mwanachuoni Mkubwa Afrika Mashariki na Kati Marehemu Shariff Sayyid Hussein Badawy, iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Jijini Zanzibar, ikiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa.(Picha na Ikulu) MWAKILISHI wa Familia ya Marehemu Mwanachuoni Mkubwa Afrika Mashariki na Kati Sayyid Hussein Badawy, ikiwasilishwa na Mwanafamilia Sayyid Mohammed Omar Al Sheikh (Judda) wakati wa hafla ya kumuombea dua baada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini