Hayo yamesemwa leo na Mwanasheria kutoka Kituo cha Misaada wa Sheria kwa Wanawake na Mratibu Uwezeshaji jamii kwenye masuala ya haki na sheria na ajira hususan kwa makundi ya vijana na wanawake, (WLAC) Consolata Kikoti wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na za umma ili kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao jijini Dar es Salaam.
Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la uelewa wa sheria na haki za wafanyakazi zinazokiukwa.
Changamoto nyingine ni usimamizi na utekelezaji wa sheria, kutokuwepo uwajibikaji katika kuhakikisha sheria hizo zinatekelezwa hasa katika taasisi.
Pia amesema vyama vya kutetea wafanyakazi vinatakiwa kusimamia haki hizo.
"Mafunzo haya ya siku moja yaliyoandaliwa na kituo cha msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) yamewashirikisha Chama cha waajiri na wadau wanaohusika na masuala ya wafanyakazi na lengo ni kuwaweka pamoja kuona namna watakavyowasaidia wafanyakazi na kusimamia haki za wafanyakazi katika maeneo yao," amesema Kikoti.
Naye, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Ilala, Vicky Kibona amesema haki za wafanyakazi zifuatwe kwani waajiri wamekuwa wakiwaachisha wafanyakazi bila kufuata utaratibu.
Amesema sheria za msingi zinazosaidia mwajiri kumsimamisha mfanyakazi au mfanyakazi kuacha kazi ni sheria ya ajira na mahusiano kazini.
"Waajiri wafuate utaratibu endapo wanataka kuahirisha kazi kwa mwajiriwa au kumsimamisha ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza," amesema Kibona.
"Wafanyakazi wengi wanaachishwa bila kufuata utaratibu na imesababisha kuwa na kesi nyingi mahakamani hivyo, ni lazima kufuata utaratibu wa kumwachisha mfanyakazi anapokuwa kazini kupata haki zake na kupunguza kuongezeka kwa kesi hizo," amesisitiza Kibona.
Windi Clement ambaye ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi SS Tanzania Limited amesema mafunzo hayo yatamsaidia kuboresha mahusiano mema kwa wafanyakazi na waajiri na kutetea wafanyakazi kuhakikisha wanapata haki zao.
Amesema viwanda vingi vinachangamoto ya mikataba kwani asilimia kubwa hutoa mikataba ya mwaka mmoja hivyo, haiwapi nguvu wafanyakazi kuweza kupambana kufanya kazi za uzalishaji.
Pia amesema uwepo wa kampuni tanzu ndani ya kampuni moja husababisha kukosekana kwa uwakilishi wa vyama vya wafanyakazi na hivyo, kusababisha wafanyakazi wengine kunyanyasika.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Ilala, Vicky Kibona,akizungumza na waandishi wa habari namna mafunzo kwa wafanyakazi kutambua haki zao za ajira kazini yatakavyokuwa na manufaa kwao. Baadhi ya wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali binafsi na zile za umma wa wakiwa katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo kutambua haki zao leo jijini Dar es Salaam.
Bundi Clement, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi kiwanda cha Pepsi nchini, akizungumza baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya siku moja kwa wafanyakazi wa a sekta binafsi na Umma ya kuwajengea uwezo kutambua haki zao za yaliyotolewa na WLAC leo Februari 12, 2021 jijini dar es Salaam.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments