Pichani ni baadhi ya wachezaji wa Namungo wakiwa nje ya basi katika karantini ya Corona nje kidogo ya jiji la Luanda nchini humo.
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeufuta mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya CD de Agosto ya Angola dhidi ya Namungo FC ya Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), sababu za kufutwa mchezo huo ni taratibu za #COVID19 ambapo mamlaka za Angola ziliutaka msafara wa timu yote ya Namungo kuwekwa karantini mara baada ya kuwasili nchini humo.
Suala kuhusu mechi hiyo litafikishwa katika kamati husika ya CAF kwaajili ya uamuzi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments